Bibianna
JF-Expert Member
- Jun 6, 2025
- 459
- 149
==
Waziri mkuu amesema kuwa Chini ya Rais Samia, mikataba minne ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) yenye thamani ya shilingi bilioni 681.53 imesainiwa mwaka 2024/25 kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wa mabasi katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).
Mikataba hiyo inahusu Awamu ya Kwanza (Kimara – Kivukoni na matawi ya Gerezani na Morocco) na Awamu ya Pili (Mbagala – Kivukoni pamoja na matawi ya Mbagala – Morocco kupitia Chang’ombe na Mbagala – Gerezani). Utekelezaji wake unalenga kuongeza ufanisi wa mfumo wa usafiri wa umma, kupunguza msongamano wa magari, na kupunguza mzigo wa bajeti ya Serikali kwa kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma muhimu za jamii.