Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,561
Mara nyingi tumesikia Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli akitajwa kumpigia simu ama Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda au Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuwapongeza ama kuwaunga mkono kwa mambo mbalimbali wanayofanya na simu hizo mara nyingi huwekwa hadharani na kusikiwa na wananchi wanaohudhuria mikutano ya wakuu hao wawili wa mikoa.
Inawezekana pia na wakuu wengine wa mikoa nao hupigiwa simu na Mheshimiwa Rais ila labda wao hawana hulka ya kuziweka simu hizo hadharani. Mheshimiwa Rais pia alishawahi kupiga simu kituo cha TV na Redio cha Clouds na simu hiyo ikasikika na wasikilizaji wa vituo hivyo.
Lakini sina kumbukumbu kama kuna siku Mheshimiwa Rais aliwahi kumpigia simu Waziri Mkuu Kasimu Majaaliwa na simu hiyo wananchi kuisikia akimpongeza ama kumuunga mkono kwenye jambo fulani. Labda pia inawezekana huwa anampigia lakini labda Waziri mkuu kutokana na ungwana alio nao hawezi kuweka hadharani mawasiliano yake na mkuu wake wa kazi. Lakini keshawahi kupigiwa simu?