ESCORT 1
JF-Expert Member
- Dec 7, 2015
- 1,436
- 3,087
Leo kituo kipya cha mabasi Nzega Mjini mkoani Tabora kimezinduliwa rasmi na Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Ujenzi wa kituo hiki cha mabasi umegharimu shiling Bilion 4.327.
Tabora wamepata stend ya kisasa waitunze sasa
Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
MAJALIWA AZINDUA KITUO CHA MABASI NZEGA MJINI
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 13, 2025 amezindua kituo kipya cha Mabasi cha Nzega mjini mkoani Tabora ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.327.
Akizungumza baada ya kuzindua kituo hicho ambacho utekelezaji wake umefikia asilimia 100, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza halmashauri hiyo kwa uamuzi wa ujenzi wa kituo hicho kwani kitaibua fursa za biashara kwa wakazi wa eneo hilo. “Kituo hiki ni kizuri na kimejengwa kwa ubora, kituo hiki kinatakiwa kianze kutumika ili wananchi waanze kunufaika nacho, Watumishi wa halmashauri ongozeni Wana-Nzega kunufaika na fursa katika eneo lenu”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri hiyo kuongeza vibanda vya wafanyabiashara badala ya vichache ambavyo vimejengwa mpaka sasa. “Tunataka wananchi wengi zaidi wanufaike, ongezeni vibanda, huu ni ubunifu mzuri sana utasababisha wengi wanufaike, waleteni wajasiriamali hapa wapate rizki zao, mkifanya hivyo mtaongeza mzunguko wa fedha”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango kazi wake wa kuwahudumia watanzania wakati wote, “Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi inaendelea kukamilisha malengo yake katika kuwatumikia watanzania ninajua hatua tuliyoifikia”.
Katika hatua nyingine, Mhehimiwa Majaliwa ametoa wito kwa watumishi wa halmashauri nchini kuendelea kujielekeza katika kutatua changamoto za wananchi “Tumueni mapato yenu ya ndani kutekeleza miradi”
Mheshimiwa Majaliwa anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Tabora.
Pia soma ~ Hivi waungwana hii Stendi ya Nzega Mjini ndio ya Sh Bilioni 4 kweli? Au mimi sijui kuthaminisha vitu!