Waziri Mkuu Majaliwa awataka Watanzania Wachangamkie soko la nafaka nchi za SADC

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1568451027540.png

Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya upungufu wa nafaka katika nchi za Kusini mwa Afrika kwa kuzalisha zaidi mazao hayo ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba zaidi.

Amesema hali ya usalama wa chakula katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), imetetereka kutokana na athari mbalimbali ikiwemo ukame katika upande wa magharibi wa ukanda, mvua zilizokithiri, mafuriko na vimbunga vya IDAI na Kenneth pamoja na wadudu waharibifu wa mazao na magonjwa.

“Athari hizo zimesababisha uzalishaji wa nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na ulezi ndani ya SADC upungue kwa asilimia 14 kutoka tani milioni 42.6 mwaka 2018 hadi tani milioni 36.8 mwaka 2019. Hata hivyo, Tanzania na Afrika Kusini kwa kipindi hicho zilizalisha ziada ya mazao hayo ambayo yanakadiriwa kukidhi mahitaji kwa mwaka 2019/2020,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuwa Agosti 29-30, mwaka huu, Wizara ya Kilimo iliratibu mkutano na wadau mbalimbali wenye kujihusisha na uzalishaji na biashara ya nafaka ili kujadili fursa zilizopo katika mazao ya nafaka, changamoto wanazokabiliana nazo na kutafuta utatuzi wake.
“Ninaigiza Wizara husika ihakikishe inashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kutumia vema fursa ya uwepo wa masoko ya nafaka kwenye ukanda huu wa SADC na hivyo, kukidhi mahitaji katika ukanda sambamba na kuboresha biashara na maisha ya wananchi wa vijijini,” amesema.

Pia ameitaka wizara hiyo iendelee kuhamasisha uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi ili nchi iweze kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada.
 
Kwa strategies NZURI za umeona nini NAMIBIA ungana na CHIKUNDE:

Strategies za kujenga miji

Strategies za kujenga shopping malls

Strategies za kujenga kilimo Bora na kuwa donor country

Strategies za kutengeneza KAZI Kwa ajili ya kuendana na life span ya reli/ndege

Strategies za kufundisha au kufanya KAZI bila recognition n.k

Strategies NZURI za kuboresha mazingira ya uwekezaji

Easy way to educate kids

[/URL]
Bro unaandika huku unatembea kwenda kuomba msamaha nini? Mbona haueleweki?
 
Wakati wanafunga mipaka nafaka zisitoke?

Wanasiasa wapuuzi sana.
 
Kilimo kitakuwa biashara ya uhakika siku serikali ikiacha siasa na kuacha nguvu ya soko iamue.
Ndio kinachofanyika kwa sasa ila je itakuwa na muendelezo au itabatilisha uamuzi baadae, hapo ndio changamoto.
 
Mtoto wangu Asha ameniuliza leo. Ile report ya kamati iliyoteuliwa na waziri mkuu kuchunguza ile ajali ya moto pale Morogoro itatolewa lini maana hadi sasa mwezi umeshapita. Nikamwambia mwanangu kamwe husiamini maneno ya mwanasiasa hata akiongea kwa unyenyekevu kiasi gani.
 
Back
Top Bottom