Waziri Mkuu Majaliwa awataka Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, pamoja na uwekezaji kuja na mkakati wa kilimo cha kisasa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,025
2,000
Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha pombe kali cha Serengeti.

Amesema mawaziri hao wanapaswa kujipanga vizuri kwa kushirikiana na sekta binafsi kuja na mkakati utakaoboresha kilimo nchini.

"Natoa maelekezo kwa mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na waziri wa uwekezaji wakae pamoja ili kuja na mkakati wa kuhakikisha wakulima wanalima kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa na rahisi."

"Wahakikishe pia wakulima wanapata mbegu bora, pembejeo na kuunganishwa na masoko ya uhakika hapa nchini, kuuza mazao yao kwenye viwanda ambavyo viko tayari kununua mazao yao," amesema.

Amesema kwa kufanya hivyo watawezesha kuongezwa fedha za kigeni na ajira nyingi kwa wananchi sanjari na kuhakikishia wakulima soko la uhakika na lenye bei nzuri.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,689
2,000
KILIMO KWANZA kiliishia wapi? Zilinunuliwa V8 VXR za kutosha kwenye huu mradi! Sijui CCM wanatuonaje watanzania? Hatuna continuity ya plans zetu kutoka awamu moja kwenda nyingine? Vipi Serikali ya Viwanda? Imepotea kama umande wa alfajiri?
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,486
2,000
Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha pombe kali cha Serengeti.
Kwa nini atoe maagizo kwenye mikutano ya Wananchi. Kwani kwenye Baraza la Mawaziri huwa wanadiscuss nini.... Anyway, arudi kwenye Kilimo Kwanza. Nasikia Kila kitu kiko pale on paper. Tatizo ni implementation.
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,284
2,000
"Natoa maelekezo kwa mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na waziri wa uwekezaji wakae pamoja ili kuja na mkakati wa kuhakikisha wakulima wanalima kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa na rahisi."

"Wahakikishe pia wakulima wanapata mbegu bora, pembejeo na kuunganishwa na masoko ya uhakika hapa nchini, kuuza mazao yao kwenye viwanda ambavyo viko tayari kununua mazao yao," amesema.

Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha pombe kali cha Serengeti.

Amesema mawaziri hao wanapaswa kujipanga vizuri kwa kushirikiana na sekta binafsi kuja na mkakati utakaoboresha kilimo nchini.

"Natoa maelekezo kwa mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na waziri wa uwekezaji wakae pamoja ili kuja na mkakati wa kuhakikisha wakulima wanalima kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa na rahisi."

"Wahakikishe pia wakulima wanapata mbegu bora, pembejeo na kuunganishwa na masoko ya uhakika hapa nchini, kuuza mazao yao kwenye viwanda ambavyo viko tayari kununua mazao yao," amesema.

Amesema kwa kufanya hivyo watawezesha kuongezwa fedha za kigeni na ajira nyingi kwa wananchi sanjari na kuhakikishia wakulima soko la uhakika na lenye bei nzuri.
Kauli za jukwaani ni za kutafuta Kiki tu, tunaviongozi walioishiwa strategies za kuongoza, wanaishi kwa kutoa kauli ambazo hazitakuwa na action yoyote baade. Kikubwa waandikwe kwenye magazeti na TV.
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,167
2,000
Kwa hiyo hatuna mkakati wa kilimo cha kisasa? Maweee!

Juzi jamaa anakataa kufanya uzinduzi kwa sababu kibanda cha mlinzi kimetumia gharama ya milioni 7. Hawa jamaa wanatudharau sana.
 
Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,042
2,000
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza Waziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na Waziri wa Uwekezaji kuja na mkakati utakaomsaidia mkulima kulima kisasa kwa kutumia teknolojia.

Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha pombe kali cha Serengeti.

Amesema mawaziri hao wanapaswa kujipanga vizuri kwa kushirikiana na sekta binafsi kuja na mkakati utakaoboresha kilimo nchini.

"Natoa maelekezo kwa mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja na waziri wa uwekezaji wakae pamoja ili kuja na mkakati wa kuhakikisha wakulima wanalima kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa na rahisi."

"Wahakikishe pia wakulima wanapata mbegu bora, pembejeo na kuunganishwa na masoko ya uhakika hapa nchini, kuuza mazao yao kwenye viwanda ambavyo viko tayari kununua mazao yao," amesema.

Amesema kwa kufanya hivyo watawezesha kuongezwa fedha za kigeni na ajira nyingi kwa wananchi sanjari na kuhakikishia wakulima soko la uhakika na lenye bei nzuri.

MWANANCHI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema mbali na kuipongeza Serengeti kwa kutekeleza adhma ya Serikali ya viwanda kwa vitendo amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili wawekeze zaidi kwenye viwanda.
 
igogondwa

JF-Expert Member
Aug 1, 2021
1,244
2,000
Kilimo cha kisasa kipi tena? Ni nani aliuwa mashamba ya maua na mbogamboga kule Arusha na Kilimanjaro? Ni nani aliharibu green houses kule Hai? Korosho mliwafanyaje wamakonde? Ngoja niendelee kujisomea PGO...
 
Vyura99tu

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
261
500
Kilimo cha kisasa kipi tena? Ni nani aliuwa mashamba ya maua na mbogamboga kule Arusha na Kilimanjaro? Ni nani aliharibu green houses kule Hai? Korosho mliwafanyaje wamakonde? Ngoja niendelee kujisomea PGO...
Endeleeni kuwaona waTanzania zuzu hawaelewi.
Kilimo cha kahawa kimefia wapi ?? Wakati soko la dunia linazidi kupaa.
Wizara zinazohusika ziko wapi na bajeti yake ikoje.
Mbolea yenyewe mtihani.
Tatueni matatizo ya wananchi acheni kuhadaa watu!!
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,909
2,000
Kilimo cha kisasa kipi tena? Ni nani aliuwa mashamba ya maua na mbogamboga kule Arusha na Kilimanjaro? Ni nani aliharibu green houses kule Hai? Korosho mliwafanyaje wamakonde? Ngoja niendelee kujisomea PGO...
Wapigania legacy hawawezi 'kuiona' hii comment yako. Ukiwaambia kuna watu walikufa kabisa baada ya kunyang'anywa korosho zao na hela ndo hawakuelewi kabisaaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom