Waziri Mkuu Majaliwa aunda kamati itakayosimamia fedha ya COVID-19 iliyotolewa na IMF

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,549
Waziri mkuu mh Majaliwa ameunda kamati itakayosimamia fedha ya COVID-19 iliyotolewa na IMF jumla ya tsh 1.3 trillion.

Mwenyekiti ni mh Jenister Mhagama.

Wajumbe ni Dr Ndumbaro, Mh Ummy Mwalimu, Prof. Kitilla Mkumbo, Dr Mwigullu Nchemba, Dr Gwajima na Mh Awesu.

Mh Majaliwa ameonya kuwa isitolewe hata senti 5 katika fedha hizi kwa ajili ya kulipana posho kwa namna yoyote ile.

Chanzo: ITV habari
 
Hii kamati ni ya hela za IMF bado ile itakayoundwa Juu ya hela za TOZO Mwenyekiti atakua PHD holder mwenyewe
 
Hamna mwanasiasa yoyote atakayeweza kumchafua Magufuli.

Kazi za Magufuli zinaonekana kwa macho ila kazi za wachafuzi hamna hata moja inayoonekana wamekalia maneno matupu tu.

Kwa hiyo huyo Zito amepoteza muda wake na heshima yake kwa jamii.
Una hangover kali sana but pole maana dunia inasonga mbele tu huku yeye alishaliwa na funza siku mingi
 
Hamna mwanasiasa yoyote atakayeweza kumchafua Magufuli.

Kazi za Magufuli zinaonekana kwa macho ila kazi za wachafuzi hamna hata moja inayoonekana wamekalia maneno matupu tu.

Kwa hiyo huyo Zito amepoteza muda wake na heshima yake kwa jamii.
Kiongozi salama huko au umepinduka na mtumbwi baharini?
 
Hamna mwanasiasa yoyote atakayeweza kumchafua Magufuli.

Kazi za Magufuli zinaonekana kwa macho ila kazi za wachafuzi hamna hata moja inayoonekana wamekalia maneno matupu tu.

Kwa hiyo huyo Zito amepoteza muda wake na heshima yake kwa jamii.
Kwani Rais gani aliyeiongoza Tanzania ambaye kazi zake hazionekani kwa macho mkuu. Huku Kusini tuna Daraja la Mkapa na Umoja. Huko Dar mna Daraja la NSSF, na Uwanja wa Mkapa na Terminal III. Kule Kigoma kuna Daraja la Malagarasi, kule machipi kuna Daraja la Ifakara. Mbona yote hayo ni maendeleo ya kuonekana kwa macho ya waliopita kabla yake. Acheni uboya yeye alitimiza yake na wengine pia.
 
Hamna mwanasiasa yoyote atakayeweza kumchafua Magufuli.

Kazi za Magufuli zinaonekana kwa macho ila kazi za wachafuzi hamna hata moja inayoonekana wamekalia maneno matupu tu.

Kwa hiyo huyo Zito amepoteza muda wake na heshima yake kwa jamii.
Unamaanisha Zito huyu mkuu au?

images (8).jpeg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom