Waziri mkuu Majaliwa atiza ahadi yake kwa wananchi wa Madaba kwa kuwaletea gari la wagonjwa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
GAR.png

Hatimaye waziri mkuu KASIMU MAJALIWA ametimiza ahadi yake aliyotoa januari 5 mwaka huu, kwa wakazi wa halimashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma ya kuwaletea gari la wagonjwa. Gari hilo limekabdhiwa na mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Magama.

Aidha mbunge huyo ameongeza kuwa wamama wajwazito watoto na wazee watabebwa bure na gari hili

Amewaonya madereva wanaowachelewesha wagonjwa kutokana na uzembe kuwa watatiwa ndani

Ni habari njema kwa mliopo maeneo hayo kwa kuwa mlikua kwenye adha hii kwa muda mrefu, ni vizuri mkatoa ushirikiano pia pale mtakapoona chombo mlichopewa kinatumika tofauti na malengo yaliyowekewa
 
Ni habari njema kwa mliopo maeneo hayo kwa kuwa mlikua kwenye adha hii kwa muda mrefu, ni vizuri mkatoa ushirikiano pia pale mtakapoona chombo mlichopewa kinatumika tofauti na malengo yaliyowekewa

Lakini serikali itupe muongozo wa sisi tunaoishi maeneo mengine ili tujue majimbo yetu yatapata lini Magari ya wagonjwa.
Maana sijajua utaratibu wa wizara ya afya mpaka sasa kutoa haya magari
 
Gari la wagonjwa kwetu inaonekana ni fadhila, badala ya kuwa ni haki ya wananchi. Ni aibu na ajabu. Hospitali nyingi za wilaya hazina huduma hiyo. Na hata hizo zinazopewa 'misaada ya ambulance', mgonjwa akiandikiwa dawa, wahudumu madirisha ya dawa na kalamu mkononi wana herufi mbili za kuandika, zikitenganishwa na mstari mshazali, o/s.
 
Mkuu hata hilo gari linahitaji service na mafuta, kitu ambacho kwa sasa hakuna hela za OC wanazopelekewa.
 
Na wasiwasi na uelewa wako, siwezi kupongeza sababu hajanunua kutoka mfukoni wake, hizi ni kodi za wananchi.
Hizo kodi za wananchi zimeanza kutolewa leo mkuu?
Kama ni kodi tu lingekuwa lilinunuliwa kitambo.

Pongeza tu hamna namna.
 
Back
Top Bottom