Waziri mkuu Majaliwa atinga bandarini na kukuta magari 44 yakitaka kutolewa kwa kutumia jina lake

Ivi ilishindikana nn mkulu alivyoenda juzi kuyagundua na hayo au iliwekwa kiporo maalumu
 
Yaani ni maigizo. Tizama Waziri Mkuu anavyokazana kuonesha yuko serious. Kumbe hata uhakika kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu imetumika kutorosha malori hana. Ndio kwanza anaagiza jamaa wakatoe maelezo.
Brother wewe haya mambo ya kikubwa huwezi kuyaelewa. Waache watu wenye weredi wayajadili. Waziri mkuu hawezi kutengeneza episode na hakuna kitu kama hicho. PM ni kiongozi wa serikali kama hufahamu. Anajua anachofanya. Watanzania mna safari ndefu sana ya maendeleo maana hamjitambui mmelala fofofo. Poleni sana. Watu wanahangaika kuwasaidia lakini ndiyi mmelala
 
mkuu-bandarini_210_120.jpg

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amebaini mpango wa kutaka kuyatoa bandarini matrela 44 ya malori makubwa, maarufu kama semitrela, bila ya kuyalipia kodi, huku wahusika wa mpango huo wakitumia jina la Waziri Mkuu.

Alibaini hayo alipofanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es Salaam, jana. Kutokana na tukio hilo, Majaliwa alimuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Simon Sirro, kuwakamata mmiliki wa kampuni ya NAS Haulage aliyetajwa kwa jina moja la Bahman na Wakala wa Kampuni ya Wallmark, aliyetajwa pia kwa jina moja la Samwel kwa kuhusishwa na njama hizo.

Pia Waziri Mkuu aliitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi, kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu serikalini. "Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu, cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu.

Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria," aliagiza. Waziri Mkuu alilazimika kufanya ziara hiyo ya ghafla jana baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuudanganya uongozi wa TPA, kutaka kutoa matrela hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka Uturuki. Bahman alitaka kupata msamaha wa kodi kwa kuidanganya TPA, kuwa amewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo, watapata matatizo.

Majaliwa alisema serikali inasisitiza watu kufuata sheria na taratibu za nchi, ikiwemo kulipa kodi ipasavyo na inataka watendaji wake wafanye kazi bila ya kubughudhiwa, hivyo aliwataka wafanyabiashara kufuata sheria za nchi na kwamba serikali haina ugomvi nao.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa mfanyabiashara huyo alitaka kuyatoa matrela hayo bila ya kukamilisha malipo ya ununuzi kutoka kwenye kampuni Serin ya Uturuki. "Magari haya aliyalipia asilimia 30 tu kwa makubaliano ya kumaliza asilimia 70 iliyobaki baada ya kufika Tanzania na atakapokamilisha ndipo angepewa nyaraka, ambayo inaonesha jina la mwenye mzigo, aina ya mzigo na thamani (bill of lading) inasaidia mteja kufanyiwa tathmini ya gharama za kulipia ushuru, lakini huyu bwana hajafanya hivyo," alisema.

Alieleza kuwa kitendo cha kuyasajili magari hayo bila ya kuwa na nyaraka hizo, ni kinyume cha sheria; na pia kinaweza kusababisha kampuni iliyouza magari hayo ya Serin kutolipwa malipo yaliyobaki. Alisema jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kudhoofisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uturuki, kwani tayari kampuni hiyo imeshawasilisha malalamiko hayo katika ofisi za Ubalozi wa Uturuki nchini.

"Uturuki wanawaamini sana wafanyabiashara wa Tanzania, sasa huu ujanjaunja uliotumika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuyasajili magari haya bila ya kuwa na bill of lading halisi, unajenga sura mbaya kwa wafanyabiashara wengine waaminifu na watiifu wa sheria, nawaagiza TRA kuchukua hatua kwa wahusika, hatuwezi kupoteza mahusiano na nchi kwa sababu ya utapeli wa mfanyabiashara mmoja," alisema.

Pia Waziri Mkuu alitoa mwito kwa mawakala wa forodha, kuhakikisha wanakuwa makini katika kazi zao na serikali haitawavumilia wababaishaji, kwani inasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo. Awali, Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimweleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na vitisho vya mfanyabiashara huyo kuwa wasipotekeleza matakwa yake watapata matatizo, lakini waliendelea kusimamia sheria na taratibu.
 
Brother wewe haya mambo ya kikubwa huwezi kuyaelewa. Waache watu wenye weredi wayajadili. Waziri mkuu hawezi kutengeneza episode na hakuna kitu kama hicho. PM ni kiongozi wa serikali kama hufahamu. Anajua anachofanya. Watanzania mna safari ndefu sana ya maendeleo maana hamjitambui mmelala fofofo. Poleni sana. Watu wanahangaika kuwasaidia lakini ndiyi mmelala

Umeitizama video? Video inaonyesha Waziri Mkuu ana uhakika? Umemsikia Mkinga, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari? Mkinga anasema Waziri Mkuu alikimbilia bandarini baada ya wafanyakazi kutilia shaka maelezo ya NAS na clearing agent, wakataka ku-verify na Ofisi ya Waziri Mkuu. Sasa wewe unachikijua ni kipi tofauti na tulichoelezwa na wahusika?

Hata kama hawezi kutengeza episode ya namna hiyo, ni dhahiri kuwa anaigiza. Kwani unafikiri waandishi wa habari aliwaita saa ngapi kurekodi ziara yake kama ilikuwa ya kushtukiza? Na unafikiri ni practical kama matukio yote ya uhalifu lazima yashughulikiwe na ama Rais au Waziri Mkuu in person? What's wrong with taaisisi husika? Kweli ndio kutusaidia kwa kuweka utaratibu kwamba taasisi zetu zitafuatilia tu yale mambo ambayo Rais na Waziri Mkuu wameagiza? Vipi wasipoagiza? Vipi kama wao wenyewe ni wahalifu? Ni lini watachunguzwa na kubainika kwa kuwa hawawezi kuagiza uchunguzi kwa mambo ambayo wanajua wanahusika. Au unafikiri wao malaika?
 
NAS ndoo Tanga Petroleum. Well connected guys. They almost ripped off Tanesco because of overchaging fuel supplies. Ally, the man himself looks to be hiding. Bahman his son is just a rabber stamp.

Ila waarabu wa Tanzania ni wapigaji sana
 
Kumuombea tu hakutasaidia sana, ni lazima yeye mwenyewe ajenge system itakayofanya kazi. Kwa mfano pale mkuu anapoonekana kumlinda na kumsifia sana mtu, anamfanya awe untouchable na wengine wanatumia mwanya huo kupiga deal tu, kama anavyosema mwenyewe sheria ni msumeno basi vyeti fake visingechagua, Angalia uvamizi wa clouds, wala hapakuwapo issue ya serikali, lakini mtu akalindwa tu Nape (ccm damu) akatemwa - unategemea nini?
Rais wetu huenda akalia sana na pengine kushikwa hata pressure, nilimhurumia sana juzi pale bandalini, anasema mpaka anafika mwisho maana hata aliowateua wanaonekana kutomsaidia - kwanini - the system is not working, imebaki mtu mmoja au wawili kama ulivyosema kwenye article yako!
Naona umenielewa,nimeweka mlolongo
wa taasisi zinazohitaji kuombewa nikasema mengine ongezea wewe
nikimaanisha kila mahali panahitaji maombi,sasa kila mtu akihitaji
maombi ni nani atamwombea mwenzie?
 
Wafanyabiashara wa magari ya kutoka Uturuki walitaka kukwepa kulipa ushuru bandarini kwa kutumia jina la Waziri wetu Mkuu Kasim Majaliwa Kasim. Cheo cha Waziri Mkuu hasa kwenye awamu hii ya tano ni kikubwa sana na kinatisha kuchezewa kama walivyofanya wafanyabiashara wale.

Lakini swali kubwa hapa ni kwanini wafanyabiashara wale hawakuogopa kulitaja na kulitumia jina la waziri Mkuu wa Tanzania kutaka kufanya uhalifu wa kukwepa ushuru?

Je, ni uhuni wao tu wa kihalifu unaostahili kuishia mahakamani?
Je, ni Kwakuwa Waziri Mkuu ana jina la kiislam kama wao?
Je, ni kweli waziri Mkuu anawafahamu kwa aina moja au nyingine wafanyabiashara hawa?
Je, ni njama za kutaka kumchonganisha Waziri mkuu na Rais wake kwa kuwa ukishatuhumiwa umetuhumiwa?
 
Itakua ndiyo jina ambalo waliambiwa "ukimtaja tu yule, mambo yanakua oya oya"
 
Na kwanini igundulike baada ya raisi kutoka bandarini asingeenda ingekuaje?
Majaliwa kasim majaliwa unamaswali mengi ya kujibu.


Kuna harufu yakafara baada ya kubuma.
 
Back
Top Bottom