Waziri Mkuu Majaliwa atembelea vituo vya kuhudumia wagonjwa wa corona ikiwemo Kibaha

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
WAZIRI MAJALIWA ATEMBELEA VITUO VYA KUHUDUMIA WAGONJWA WA CORONA

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Hospitali ya Wilaya ya Kibaha iliyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika na kuwa na maambukizi ya COVID19 ni kituo cha tatu

Vituo vingine ni Temeke Isolation and Treatment Centre, Treatment Centre karibu na Hospitali ya Mloganzila. Amesisitiza kuwa Temeke bado hakujajaa

Hospitali hiyo ya Kibaha ilitembelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jumamosi Machi 28, 2020 ambaye alibainisha kuridhishwa na maaandalizi
 
Mpaka hatua ya ugonjwa ulipofikia bado wanaongelea maandalizi? Athari ya kweli inafichwa. Kwa janga hili ndipo ule usemi wa mficha maradhi kifo humuumbua itabainika. Mungu atunusuru tu.
 
Dar es salaam na Kibaha, Vp kule Kigoma, Kagera, Mtwara, Lindi, Tanga, Singida, Rukwa nk maana kila siku tunazungumzia vituo vya Dar na hapo Kibaha..
 
Back
Top Bottom