Waziri Mkuu Majaliwa ataka viongozi Afrika kusimamia madini

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
MAJALIWA-.jpg

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani) amesema mataifa ya Afrika yanatakiwa yaandae maarifa, vitendea kazi na rasilimaliwatu watakaoweza kusimamia na kuendeleza ipasavyo sekta ya madini na kuleta tija kwa Taifa husika na wananchi kwa ujumla.

Amesema taarifa za kijiolojia zinaonesha kuwa Afrika ni bara lenye utajiri mkubwa wa rasilimali madini huku sehemu kubwa ya madini hayo yakiwa bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana alipofungua Mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa kituo hicho mkoani Dar es Salaam.

Alisema rasilimali za madini zilizopo Afrika zinaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi nyingi iwapo itasimamiwa vizuri. Alitolea mfano Tanzania ambayo licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, almasi, chuma, madini ya vito kama tanzanite, lakini mchango wa sekta ya madini ni asilimia 4.8 ya pato ghafi la Taifa.

Waziri Mkuu alisema kituo hicho kikitumika vema kwa mujibu wa kusudi la uanzishwaji wake kinaweza kuleta tija kubwa kwenye sekta ya uchumbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta. Alisema kituo hicho ni moja kati ya taasisi chache duniani yenye teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kusaidia kufanya uchambuzi wa miamba na madini yaliyomo.

“Pia ni sehemu ambayo unaweza kupata huduma za ushauri na kusaidia teknolojia utakayoweza kutumia ili kufanya uzalishaji wa madini mbalimbali,” alieleza. Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali; ya wanachama kutolipa ada kwa wakati na ya wanachama wa kituo hicho kutokitafutia wateja na masoko. Pia miundombinu mingi ya kutuo ni chakavu. Akizungumzia changamoto hizo, Waziri Mkuu ameziagiza nchi zote zinazodaiwa ada ikiwemo Tanzania zilipe ada stahiki kwa wakati na kuweka mkakati wa kukitangaza kituo hicho ili kukiwezesha kupata wateja kwa ajili ya kutumia huduma zitolewazo.

Habari Leo
 
Hawata tuacha salama hao.
Lakini inabidi Africa tuwe wamoja na kuhakikisha tuna saidiana hata kama hatuna wataalamu tuwalete toka nchi zingine za Africa na sio vinginevyo
 
Back
Top Bottom