Waziri Mkuu Majaliwa apiga marufuku mikutano ya kisiasa

Mzee Mchopu

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
1,031
268
Kwa kile kinachoitwa mshtuko Waziri mkuu MAJALIWA KASSIM MAJALIWA leo Apiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kuwashukuru wananchi hasa kwa wale wagombea walioshindwa uchaguzi.

Nini tafsiri ya hii kitu? Kwa haraka haraka ninavyohisi huu UTAWALA utakuwa ni moja kati ya utawala ambao UTAWALA BORA umewekwa mfukoni na kuongozwa kwa Proclamations and Decrees,Which is not good.

NACHUKUA NAFASI HII KULIKEMEA HILI kwa majina yote
 
Cowardness nothing else.
Serikali inagharimia hii mikutano?
Nami nakemea kwa nguvu zote.
PM acha woga usio na sababu.
 
Kama mwendo ndio huu basi mgema akisifiwa tembo hulitia maji!
Nahisi hata makongamano ya kidini yatapigwa marufuku!
 
kwa kile kinachoitwa mshtuko
Waziri mkuu MAJALIWA KASSIM MAJALIWA leo Apiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kuwashukuru wananchi
Hasa kwa wale wagombea waloshindwa uchaguzi

Nini tafsiri ya hii kitu
Kwa haraka haraka
Nnavyohisi huu UTAWALA utakua ni moja kati ya utawala ambao UTAWALA BORA umewekwa mfukoni
Na kuongozwa kwa Proclamations and Decrees
Which is not good

NACHUKUA NAFASI HII
KULIKEMEA HILI
kwa majina yote

Mwehu wewe! Kama hujui usemacho bora unyamaze kuliko kuleta uongo. Hakusema watu wasiwashukuru waliowachagua
 
Waziri Mkuu yuko Lindi na anazungumza na wapiga kura jimboni kwake kwenye mikutano ya hadhara. Je hiyo siyo ya kisiasa na kuwashukuru?
 
Asante muh.Kasim Majaliwa. Tuache upuuzi Wa kushukuru. Tujenge nchi. Wazungumze bungeni au kuitisha press conference.

Ulaya na marekani uchaguz ukimalizika, hakuna mikutano ya kisiasa. Siasa huhamia bungeni, kwenye makongamano au mkutano na waandishi Wa habari.

Hongera Waziru Mkuu

Unayajua majukumu ya vyama vya siasa
Umeshawahi kuisoma sheria ya vyama vya siasa

Halaf tambua hapa si ULAYA


MNAOGOPA NN hasa yule mzee huenda aliwashinda kweli maana hiz nguvu si bure
 
Mwehu wewe! Kama hujui usemacho bora unyamaze kuliko kuleta uongo. Hakusema watu wasiwashukuru waliowachagua

Mkuu nina akili timamu na sjaandika kishabiki nimetoa hisia zangu
Kasema wale waloshinda ndo watashukuru ila kwa walioshindwa hawana nafasi hizo zaidi ya kutuvuruga na huu ni wakati wakazi

Huu unaweza tafsirika kama ubaguzi kwan itaonekana kuna tabaka fulan ndo linastahili kupata haki zote na jingine haliruhusiwi
Sio vizuri
Huenda PM aliteleza
Msemaji wa SERIKALI AJITOKEZE
ALIWEKE SAWA!
 
Chanzo cha habari yako ni kipi? Naangalia taarifa ya habari ITV, habari za kitaifa zimeisha sijaona habari yako hii ai nisubiri za kimataifa?

Aaaahhh nimecheka kwl! Labda tusubiri za michezo au kibonzo cha leo.
 
Walioshinda waende wakashukuru, na walioshindwa waruhusiwe wakawalaumu wapiga kura wao.
 
kunya anye kuku akinya bata kaharisha teh teh teh kama ana bora afute vyama vingi wamtangaze shein
Waziri Mkuu yuko Lindi na anazungumza na wapiga kura jimboni kwake kwenye mikutano ya hadhara. Je hiyo siyo ya kisiasa na kuwashukuru?
 
Walioshinda waende wakashukuru, na walioshindwa waruhusiwe wakawalaumu wapiga kura wao.

Viongozi wengi katika kipindi wataendelea kufanya kazi juu ya sheria.Nadhani nchi haitaendeshwa kwa operation za kijeshi ila kwa "Utawala wa Sheria"
 
Kama ni kweli basi na yeye atakuwa jipu la aina yake. May God forbid.
 
Back
Top Bottom