Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Uwanja wa Fisi paboreshwe

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,458
99,094
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kuboresha eneo maarufu la Uwanja wa Fisi lililopo Magomeni ili liwe safi na kubadilisha historia ya eneo hilo.

Majaliwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kinondoni mkoani hapa ambapo amezungumza na viongozi na kutembelea Mto Ng'ombe katika kata ya Tandale.

Akizungumza na viongozi wa Kinondoni, Majaliwa amesema eneo hilo limekuwa chafu na mvua inaponyesha hali inakuwa mbaya zaidi, maji yanatuama na kutengeneza tope.

"Kwani kuna ubaya gani eneo lile likiwa safi! Liko ndani ya halmashauri yenu, wekeni mkakati wa kuliboresha, pengine hata jina litaondoka lenyewe litapata umaarufu zaidi," amesema Waziri Mkuu.

Majaliwa amesisitiza hilo wakati akizungumza na wananchi wa Tandale akisema lijengwe vizuri, watu wafanye biashara zao vizuri na manispaa iweze kukusanya mapato.

"Kwani kuna tatizo gani eneo la Uwanja wa Fisi likifungwa taa ili ikifika usiku tuwe tunaonana?" amesema Waziri Mkuu huku akishangiliwa na wananchi wa eneo hilo.

"Pale kuna watu wafanyabiashara, wawekewe mazingira mazuri, wapate leseni, wafanye biashara zao. Liwe ni eneo zuri la biashara," amesema Majaliwa.

Eneo la Uwanja wa Fisi lilipata umaarufu kutokana na biashara ya ukahaba iliyokuwa ikifanyika katika eneo hilo, jambo ambalo lilikuwa likilalamikiwa na wakazi wa maeneo ya jirani.

Mkazi wa Tandale kwa Mtogole aliyekuwa akimsikiliza Waziri Mkuu, Mwanaisha Baraka amesema amelifahamu eneo hilo kwa muda mrefu na kwamba kwa sasa vitendo vya ukahaba vimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma.

"Uwanja wa Fisi ilikuwa zamani, siku hizi pako vizuri. Bora wajenge soko, itasaidia kukomesha kabisa biashara ya ngono," amesema mwananchi huyo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Vile vyumba ni vidogo sana, mkiingia wanaume wawili watatu mkaacha jasho lenu hata ubani hautoshi kuitoa harufu ya kijasho.

Waziri mkuu angetumia fursa hiyo kuwaasa wamiliki wa vijumba vile wapanue kidogo.
Kama ameshindwa basi bei elekezi ipande walau kwa sh 2000.

Palinifaa sana hapo.
 
Vile vyumba ni vidogo sana, mkiingia wanaume wawili watatu mkaacha jasho lenu hata ubani hautoshi kuitoa harufu ya kijasho.

Waziri mkuu angetumia fursa hiyo kuwaasa wamiliki wa vijumba vile wapanue kidogo.
Kama ameshindwa basi bei elekezi ipande walau kwa sh 2000.

Palinifaa sana hapo.
Kwahiyo amesema wanaboresha ili mnyanduane vizuri?
 
Zamani nkitaka kutoka kwenda piga mtungi nlikuwa naenda huko maana ilikuwa kama nakwenda mbugani kutalii
Ukikaa huyu kakabwa,kule ngumi,huyu kafumaniwa yaani burdan

Ova
 
Back
Top Bottom