Waziri mkuu Majaliwa aagiza hospital ya Uhuru mjini Dodoma iwe imekamilika ndani ya siku 15 ili Rais Magufuli aifungue 09/12/2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Waziri mkuu ametembelea kwa ghafla hospital ya Uhuru iliyopo Chamwino mkoani Dodoma na hajaridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wake.

Akiwa amekasirishwa mh. Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya siku 15 ili mh. Rais Magufuli aje aifungue siku ya sherehe za Uhuru yaani 09/12/2020.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa hiyo iharakishwe kukamilika ili Rais aizindue tarehe 9/December!

Hizo ni akili au matope?

Hospitali inapaswa kujengwa kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi na sio kufikia matamanio ya kuzinduliwa na mtawala ili kumpa sifa.

Serikali itoe pesa, wakandarasi wa uhakika wawepo kazini na wataalamu wapewe nafasi ya kufanya kazi zao pasipo kukimbizwa.
 
Sasa kwani Hospital inajemgwa kwa ajili ya Mifugo? Hivi unafikili PM kakurupuka kusema hivyo! ,Unajua hiyio hospitality ilipangwa ikamilike lini na sasa imefikia hatua ipi? Msipende kukimbilia kupinga Kila kitu !.Mnaonekana hamna akili ni Bora kukaa kimya tu!.
 
Hayo Ni maigizo ya kisiasa. Tatizo pesa za malipo kwa wakandarasi hazitolewi kwa wakati.

Mkataba ujenzi unawakati wa kuanza na kuisha ikiwa mkandarasi hajakamilisha kwa wakati mkataba unavunjwa na kutafutwa mwingine.

Kwa siasa hizi ujenzi unaweza kuwa chini ya kiwango au ipo siku jengo kudodondokea wagonjwa na wafanyakazi.
 
Siku 15? Mmmh
Bora hata ww umestuka. Yaani mtu atembelee jengo kisha atoke hajaridhishwa kabisa, lakini atoe siku 15 ujenzi uwe umekamilika! Nijuavyo mimi siku 15 ni kwa ajili ya kufunga taa na kuweka alama za vibao, na sio jengo ambalo hajaridhika kabisa. Magu asipoangalia atamfanya huyo PM awe mwendawazimu.
 
Back
Top Bottom