Waziri Mkuu: Mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora Serikali iyauze kuliko kuyaacha yakiozea pale yard

Hata mimi nashangaa kwa kweli.

Kinachoshangaza ni huo ushauri anaotoa Waziri mkuu kuwa hayo mabasi yauzwe, watamuuzia nani? Hayo mabasi yalitengenezwa kutembea kwenye hizo barabara maalum sasa mkimuuzia mtu binafsi atayaendesha wapi? Hayo mabasi mabovu pengine yawe cannibalized na vipuri vitumike kwenye hayo magari yanayotembea badala ya kuagiza spea toka nje!! Mabaki mengine ya chuma yanaweza kuuzwa kama chuma chakavu.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa ameshauri mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora yauzwe kuliko kuyaacha yakioza pale yard

Waziri mkuu amesema hayo baada ya kushuhudia mabasi takriban 50 yakiwa yamelala kabisa kwa ubovu na yakizidi kuchakaa.

Chanzo: ITV habari

Ramadhan Kareem!
Afu wewe ni kama huna kazi zaidi ya kukaa lumumba na kuangalia tbc kumeza na kuandika habari za mataga humu jf
 
huu mradi wangepewa watu binafsi waendeshe kibiashara au wengeruhusu wenye daladala kununua share tuone kama kutakuwa na haya mambo, halafu magari hayo yalikuwa ni used, pili njia za bongo changamoto sana angalia maji jangwani pale!?

hivi mtu akinunua atayatumia wapi!?
Hapo nimekuelewa mkuu. Mfano mzuri ni BRT za Dubai pamoja na Metro zao. Road Transport Association(RTA) ya serikali hiyo ina manage kwenye maofisi huko lakini ukiingia ground penye kazi, kila kitu kimewachiwa kampuni ya Serco Group Plc. Hao jamaa ndio operators wa mabasi, metro, kwenye airports pia wapo na ni kampuni kubwa sana inayo manage zaidi ya contracts 500 duniani, sehemu tofauti tofauti hadi za kijeshi.

So, deal ka hizo zikihusishwa private sector wapewe shares pia, wenye kutoa services zipatiwe kampuni inayoaminika ya Bongo. Serikali ikuwe pale juu, ku manage kila kitu, kuanzia progress hadi hela yake. Ingekuwa bora.
NB;that's my opinion, if am wrong you're free to correct me. ✌️
 
Yatapita njia gani?
Hilo ndilo swali la msingi.

Inajukikana wazi hata na yeye mwenyewe PM analielewa hilo, kuwa hayo mabasi ni "special" kwa njia maalum ya mabasi ya mwendokasi

Je yeye PM anavyowashauri hao mwendokasi kuwa ni bora wangeyauza hayo mabasi, je yatapita njia gani??
 
Hivi Rais akifia madarakani waziri mkuu nilazima aendelee yule aliyekuwepo??

Siyo lazima ni maamuzi ya Rais mpya !
Lkn waziri mkuu akiwa mwaminifu , anaejali maslahi ya taifa huku skichapa kazi usiku ns mchana rais hana budi kumruhusu aendelee
 
Nani atanunua mibasi mobovu ile Majaliwa anafikiri kuuza yale ni rahisi ? Hakuna mnunuzi wapambane wafufue au watupe wauza chuma chakavu......uliona uda imeuzwa kwa raia kawaida?
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Mradi ulianza 2016
 
Duh!auziwe nani na akataye nunua atayatumia wapi?

Ova
labda atakayenunua apewe access ya njia hiyo
itakuwa kama railways companies south africa , kuna makampuni kadhaa tofauti tofauti lakini yanatumia railway track moja ,
serikali ikubali tu haiwezi kufanya biashara , wawape sekta binafsi waendeshe huo mradi hata partially majibu yataonekana
 
Back
Top Bottom