Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,204
- 42,064
Baada ya kuungua kwa Soko la kariakooo yalisemwa mambo mengi ikiwemo hujuma au kuunguzwa kwa makusudi kwa soko husika. Lakini Waziri Mkuu aliunda Tume ya Uchunguzi na akawapa maagizo ya kumletea report ndani ya wiki mbili.
Kama ilivyo ada report iliwasilishwa ndani ya wiki mbili => Waziri Mkuu apokea taarifa ya Uchunguzi wa Moto soko la Kariakoo
Lakini baada ya kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu, matarajio ya wengi kama alivyoahidi ni kutoa report hiyo kwa Umma kuhusu kilichosababisha soko kuungua.
Pamoja na hayo yote ikumbukwe Waziri mkuu alishatoa tuhuma kwa watu kuhujumu soko hilo wakiwemo waliokuwa viongozi wa soko la Kariakoo waliofukuzwa na Rais Samia Suluhu kabla ya soko kuungua.
Watanzania walikuwa na hamu sana kujua nini kilisababisha soko hili kuungua. Kwanini Waziri mkuu ameficha hii report? Haina majibu aliyoyatarajia? Amezuiwa kuisoma?