Waziri Mkuu, kuwa Makini sana na Waziri Mwambe

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
WAZIRI MKUU MAJALIWA, KUWA MAKINI ZAIDI NA WAZIRI MWAMBE. AMEJAA KIBURI, CHUKI, NA MPENDA RUSHWA

Katika mabadiliko madogo aliyoyafanya Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan alimtoa Mwambe kwenye wizara ya Viwanda na Biashara na kumbadilisha na Prof. Kitila Mkumbo, ambapo Mwambe akahamishiwa katika wizara ya Uwekezaji ilio chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Tukiwa tunaanza ukurasa mpya, chini ya awamu hii mpya ya Mama yetu shupavu, basi Waziri Mkuu Majaliwa pokea dondoo hizi kuhusu Mwambe, kijana aliyeletwa chini ya ofisi yako...

Mwambe ni mtu wa chuki iliokithiri. Katika awamu ya tano kuwa kwake karibu na Doto James (aliyekuwa KM Hazina) ilimfanya Mwambe kujaa kiburi, kuwa na chuki na majivuno makubwa sana. Kwa hakika naye alikuwa katika kundi la watoto pendwa wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano. Kuwa kwake karibu huko kulimfanya afanye maamuzi ya ovyo, na yenye chuki hasa alipokuwa kama Waziri wa Viwanda na Biashara. Japo ni kwa muda mfupi ila alivuruga wizara yote na taasisi zake. Leo hii Prof. Kitila Mkumbo anakuja kuanza kazi upya.

Kwa muda mfupi Mwambe alijenga chuki, aligombana na hata kugombana na wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya wizara na hadi kuwatoa baadhi Ma-DG na kufanikiwa kuweka wake hata ambao hawakuwa na sifa kinyume na taratibu na sheria za utumishi.

Mwambe alifanikiwa kuweka ambao hawana uwezo. Moja ya kikao cha Management, katika moja ya taasisi alinukuliwa akitishia watumishi na kuwaeleza ni kwa namna gani ana nguvu kubwa sana kwa Rais JPM na anaweza kufanya lolote lile kwa muda wowote ule bila kuulizwa. Alidiriki kutishia kufuta baadhi ya taasisi chini ya wizara hiyo hata zile zilizoanzishwa kisheria.

Sio, hivyo tu. Mwambe pia ameendelea kujitapa kuwa hata Rais wa sasa Mh. Samia Suluhu Hassan anamudu ipasavyo, na hawezi mfanye lolote. Amenukuliwa mara kwa mara akisema hayo. Ingawa ukweli sio huo, kwani katika dhifa zote mbili ya Ikulu - Chamwino na Ikulu- Dar es Salaam tumeshuhudia Rais. Samia akimshambulia Mwambe, na hata sababu kadhaa anazozijua ndio zimempelekea ahamishwe wizara. Juzi wakati wa uapisho wa Makatibu Wakuu, Mh. Rais alimshambulia tena na kudiriki kusema wazi ni namna gani Mwambe ameshiriki kuleta ukiritimba na kudidimiza uwekezaji hapa nchi, kwani alipokuwa TIC kama Mkurugenzi alishiriki kutunga kanuni na kuweka utaratibu zilizokandamiza wawekezaji hapa nchini.

Waziri Mwambe alipokuwa wizara ya Viwanda n Biashara alishutumiwa kupokea rushwa ya Mln. 50 kutoka kampuni moja (jina tumehifadhi kwa sasa, ingawa tumekutumia Waziri Mkuu kama barua ya siri). Lengo kuu ilikuwa ni kubadilisha status ya shareholders kinyume na utaratibu za usajili wa Makampuni. Kwa Mamlaka aliyokuwa nayo alijaribu kulazimisha bila mafanikio mpaka mabadiliko yalipomkuta chini ya Rais Mh. Samia Suluhu Hassan. Hata baada ya kifo cha Hayati Magufuli, Mwambe alijaribu kubadili status hiyo ya shareholders akilazimisha yafanyike mapema kabla ya Rais mpya kupangua baraza la mawaziri. Ni kama vile alijua kuwa hatoweza kurudi katika wizara ya Viwanda na Biashara.

Wakati wa mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika Ikulu Dar es Salaam chini ya Hayati Rais Magufuli alijaribu kimchonganisha Mh Lukuvi kuwa analeta ukiritimba katika kugawa ardhi baadae ikaonekana waziri wa ardhi alikuwa sahihi kwamba hio kampuni aliyokuwa anaitetea waziri mwambe walikuwa madalali

PM Majaliwa huyu ndiyo Mwambe ambaye kwa sasa kaletwa chini ya ofisi yako. Ni wazi utawala uliopita Mwambe alikuwa ashikiki, na ni wazi alipata nguvu kutoka kwa Rais. Magufuli.... Amekuwa akijitapa kuwa ni yeye pekee katika nchi hii aliyeambiwa na Rais Magufuli kuwa chagua wizara yoyote ile au kazi yoyote ile nikupe, hii akionyesha watu ni kwa namna gani Rais aliyepita alikuwa anamwamini.

Yakiwa ni matumaini yetu, kwa mabadiliko haya yaliyofanyika, pia kama wadau katika wizara hii basi tuchukue fursa hii kumpongeza Rais wetu mpendwa Mama. Samia Suluhu kwa kufanya mabadiliko katika hii wizara. Prof. Kitila Mkumbo karibu sana na njoo uanzie alipoharibu Mwambe, kiukweli kafanya uharibifu mkubwa sana ndani ya wizara na katika taasisi zake zote, sio tu morale ilishuka bali kwa muda mfupi huu aliongoza taasisi kwa chuki, kiburi, majivuno na amri hata kwa zile zilizopelekea kuvunja sheria na taratibu ndani ya wizara.

Prof. Kitila chukua muda, tembelea idara zote ndani ya wizara. Tembelea taasisi zote ndani ya wizara utakutana na malalamiko makubwa sana ya namna gani wizara iliharibiwa na Mwambe.
 
Mwambe ni chawa, CCM ile ile ambayo wanamdharau mama na kuishi maisha ya mwendazake
 
Mwambe ni kijana very humble hata haya ya ukiritimba na wawekezaji kusumbuliwa alikemea sana tangu yupo TIC.

Labda kama kabadilika leo!
 
Mkuu heshima yako!

Pamoja na maelezo meengi ya malalamiko juu mchumi Mwambe, ila nimeshangaa sana kuna baadhi ya aya umesema Mwambe akibadilisha wakurugenzi na kuwaweka wasio na uwezo. Sawa yaweza kuwa kweli, kwa nini sasa umeshindwa hata kuwataja baadhi ya wakurugenzi ambao hawana uwezo waliowekwa na Mwambe?

Well, umemchongea sana bwana Mwambe kwa Mh. Rais ila ni Mwambe huyu huyu ambaye alikuwa anakataa Biashara zisifungwe kutokana na kodi za TRA na ni Mwambe huyu huyu amekuwa akisisitiza Watumishi wa Serikali wanatakiwa kuwa-engage wafanyabiashara na sio kuwabambikia makodi na kufunga na Biashara kwa sababu kuna wazalishaji wengine wanalipa kodi kila siku.

Umesema Mh. Rais alimsema Mwambe kuwa ameharibu wizara ya Uwekezaji kwa kuweka ukiritimba, sasa kwa nini hakumuacha? Nakumbuka Mh. Rais akisema anamrudisha Mwambe Uwekezaji kwa sababu ya professional yake na alifanya vizuri akiwa TIC!

Turudi kwa Ndugai anayesema kuna wabunge wa Lindi na Mtwara wameenda kumlalamikia, kwanzw tujiulize wamelalamika kuhusu jambo gani? Je, awapendelee kwa jambo lolote? Au awape fedha? Kumbuka Mwambe ni mbunge na ni waziri pia, hivyo huwa anashiriki vikao vya wabunge wa Lindi na Mtwara kama mbunge na hata last time akishiriki kikao cha wabunge wa Mtwara kuhusu kero ya umeme ambapo walikuwa na waziri wa Nishati. Na kama kweli wabunge wa Lindi na Mtwara wamelalamika kwa Spika, Je spika alishawahi kumuita Mwambe na kuongea kuhusu hili?

Mwisho; Bahati mbaya sana Mh. Mwambe sio mwanasiasa wa maneno maneno meeengi, ila amekuwa akijipambanua kama mtendaji mwenye kuleta solutions muda wote.

Lingine ingawa sio kwa Umuhimu, Mwambe ni 'very humble guy' kuna ile demotion aliipata kutoka kuwa Mkurugenzi wa Idara moja wapi kwenye Wizara ya Mambo ya Nje mpaka kwenda kuwa DC-Manyoni, lakini aliendelea kupiga kazi bila manung'uniko na hatimae kupewa Ukurugenzi wa TIC kabla ya kwenda kuwa Mbunge na baadae kuteuliwa kuwa waziri.

Wqbongo tunapenda majibu maneno maneno na uongo uongo mwingi, hatupendi kuambiwa Ukweli!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom