Waziri Mkuu kutoongelea zao la kahawa Karagwe ni makusudi au bahati mbaya?

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
880
843
Leo waziri mkuu Kasimu Majaliwa ametembelea wilaya ya Karagwe, wakati anahutubia hajagusia roho ya uchumi wa wilaya ya Karagwe - kahawa. Bila maendeleo ya zao la kahawa, hakuna maendeleo ya wilaya.

Kuna matatizo mengi juu ya zao la kahawa, bei mbaya, tozo za kila aina, wizi wa vyama vya ushirika, kutopata ushauri wa kitaalam juu ya kilimo Cha kahawa, madeni ya vyama vya ushirika.

Vitu vyote alivyoongelea, umeme, hospitali, Barabara, vyuo (elimu). Haviwezi kwenda bila kufanya mageuzi ya maendeleo ya jumla ya zao la kahawa. Walio karibu naye mfikishie ujumbe
 
Huwa najiuliza sanaa, anapokuja kiongozi mkuu kwenye Wilaya, kijiji, kata au mkoa hivi ni kweli kabisa huwa mnaamini huyo mtu mmoja ndiye atawaletea mabadiliko?

Yaani mfano kuna wezi baina yenu (sijui ushirika, vyama vya msingi etc etc) nyie mmeshindwa kuchukua hatua, tena kwa sababu za kipuuzi tuu (kujuana, kada mwenzenu etc) halafu eti mnataka akija kiongozi wa juu ndiye aje na solution, really?? Hata kama ni mimi nawapotezea tuu mpaka akili ziwarudi.
 
Leo waziri mkuu Kasimu Majaliwa ametembelea wilaya ya Karagwe, wakati anahutubia hajagusia roho ya uchumi wa wilaya ya Karagwe - kahawa. Bila maendeleo ya zao la kahawa, hakuna maendeleo ya wilaya...
Mkuu KADERESI ni nani huko
 
Huwa najiuliza sanaa, anapokuja kiongozi mkuu kwenye Wilaya, kijiji, kata au mkoa hivi ni kweli kabisa huwa mnaamini huyo mtu mmoja ndiye atawaletea mabadiliko? Yaani mfano kuna wezi baina yenu (sijui ushirika, vyama vya msingi etc etc) nyie mmeshindwa kuchukua hatua, tena kwa sababu za kipuuzi tuu (kujuana, kada mwenzenu etc) halafu eti mnataka akija kiongozi wa juu ndiye aje na solution, really?? Hata kama ni mimi nawapotezea tuu mpaka akili ziwarudi.
Waziri mkuu ana jukumu kubwa la kulinda masilahi ya wananchi wake. Matatizo mengine yanasabishwa na sera za watawala. Sera ya CCM wanasema ni kulinda ushirika, ambao ndiyo wezi ninaosema.

Serikali imezuia wanunuzi binafsi ili kulinda ushirika. Ushuru wa halmashauri, ambao wako chini ya waziri mkuu, unashusha bei ya kahawa. Halmashauri wameachwa wanaweka ushuru mkubwa ambao unamuumiza mkulima.

Serikali inapaswa kuajiri wataalamu wa kilimo, wawasaidie wakuluma utaalamu wa kilimo. Mkulima ameachwa kama yatima. Hana msaada anaopewa, anahangaika peke yake wakati wa kulima, akivuna anapangiwa bei na ushuru kibao juu yake.
 
Apunguze tozo juu ya bei ya kahawa, akemee wezi wa ushirika wanaolindwa na sera za CCM, aruhusu ushindani wa wanunuzi binafsi, aajiri wataalamu wa kilimo. SI ndiye serikali yenyewe!
Ni mawazo mazuri sana. Naunga mkono hoja. Bahati mbaya CCM hawawezi kufanya hayo, si kwamba ni mabaya ila sababu hawafanyagi hivyo, yaani siyo business a usual kufanya hayo.

Pia bahati mbaya sana wapinzani hawajajua nguvu wanayoweza kupata kwa kutetea wakulima. Siku kikitokea chama cha siasa kikamtetea mkulima wa nchi hii dhidi ya tozo, ushirika, restriction ya kuuza nk, kitapata nguvu kubwa sana.
 
Apunguze tozo juu ya bei ya kahawa, akemee wezi wa ushirika wanaolindwa na sera za CCM, aruhusu ushindani wa wanunuzi binafsi, aajiri wataalamu wa kilimo. SI ndiye serikali yenyewe!
Mkuu KADERESI huko Karagwe ni mali ya nani...
 
KADERES ni taasisi binafsi inayonunua mazao ya organic. Naye anaruhusiwa kununua kutoka ushirika (KDCU) kwa nguvu
Great!! Nilikuwa huko mna ardhi nzuri saana na landscape nzuri tu....chakula cha kutosha ila nilipo fuatilia bei ya Kahawa na Majirani nzenu ni mbingu na dunia.

Vipi ile Ranch kabla ya kufika au kupanda juu Karagwe kutokea BK mjini Nani miliki?
 
Zamani ilikuwa ya NARCO, sasa hivi sehemu imebinafsishwa kwa Kagera sugar na nyingine ilichukuliwa na marehemu raisi.
Tunalalamikia bei ya kahawa kwa sababu jirani zetu - Uganda mpaka 3,000. Ila unazuiwa usiwauzie. Hatuna soko huria. Bei anapanga mkuu wa mkoa. Ni hatari. Wakulima wanajitahidi ila wanaangushwa na mfumo wa utawala
 
Mbona taarifa imetolewa kuwa Waziri mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuunda tume ya kufatilia bei ya kahawa au wewe hukuwepo
 
Badilikeni wanakaragwe. Dunia ya leo nani anakunywa kahawa ambayo ina chembechembe za caffeine??

Vinywaji mbadala vipo kibao. Kahawa haitakuja kuwa na soko milele.
 
Zamani ilikuwa ya NARCO, sasa hivi sehemu imebinafsishwa kwa Kagera sugar na nyingine ilichukuliwa na marehemu raisi.
Tunalalamikia bei ya kahawa kwa sababu jirani zetu - Uganda mpaka 3,000. Ila unazuiwa usiwauzie. Hatuna soko huria. Bei anapanga mkuu wa mkoa. Ni hatari. Wakulima wanajitahidi ila wanaangushwa na mfumo wa utawala
Hapo kwenye kupanga bei..kuna kitu hapo pia si watu waruhusiwe kuuza uganda SOKO HURIA
 
Badilikeni wanakaragwe. Dunia ya leo nani qnakunywa kahawa amabayo ina chembechembe za cocaine??

Vinywaji mbadala vipo kibao. Kahawa haitakuja kuwa na soko milele.
Uganda lipo soko na bei iko juu ila wamezuiwa kuuza huko
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Uganda lipo soko na bei iko juu ila wamezuiwa kuuza huko
Monopoly ni sera ya kila nchi ktk dunia ya leo. Kwahiyo hata kama leo kuna soko la kahawa huko Uganda, haliwezi kuwa toshelevu na endelevu.

Mwisho wa siku kahawa yao ikipungua bei kwasabb ya kahawa ya Tanzania kuingia nchini mwao wataizuia ya kwetu.
 
Mbona taarifa imetolewa kuwa Waziri mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuunda tume ya kufatilia bei ya kahawa au wewe hukuwepo
Tatizo la wanasiasa ni hata tatizo linalojulikana ni kupiundia tume. Suruhu Iko wazi.
1. Ukiritimba _ waruhusu soko huria. Wanunuzi washindane, mwenye bei ya juu ndiye anunue. Hii ya kulazimisha KDCU ndiye mnunuzi pekee Inawagamya wanunue kwa bei wanayotaka.
2. Ushuru wa halmashauri uko juu. Kuna Kodi nyingi kwa kila kilo ya kahawa. Wakati huo halmashauri inamchango mdogo kwa wakulima.
3. Usimamizi wa KDCU. Kama kweli sera ya CCM ni kulinda ushirika, basi simamieni uendeshaji wake. Wana gharama za uendeshaji zisizo na tija( administration expenses), kuna wizi kuanzia kwa madreva wanaosomba mpaka huko juu. Angalia kwa msimu mmoja vijana wanaofanyakazi mle wanajenga majumba, wananunua magari ......

Mkulima tangu anapanda kahawa mpaka anavuna, huoni mkurugenzi, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa wala OCD, ila kahawa ikiiva na kuvunwa, angalia magari ya Mkurugenzi, OCD mpaka mkuu wa mkoa yanavyopishana kuzuia kahawa isiuzwe magendo. Nguvu hiyo ingetumika tangu kahawa inapandwa mpaka inavunwa, tungepata mazao ya kutosha.

Haya yanajulikana, je kuna haja ya kuundiwa tume?
 
Kagera mnachakujifunza wakati wa KAMPENI
 
Hana cha kuzungumza kuhusu kahawa maana aliwazuia wanyambo hata kutafuna kamwani
 
Back
Top Bottom