Waziri Mkuu kutajwa kwenye pembejeo feki ni bahati mbaya au wamekosea?

Mtu wa Asali

Senior Member
May 9, 2022
152
291
Shaka huna nguvu ya kupambana na wauzaji wa Pembejeo feki mtwara ni michezo wameshaizoea.

Nimeshangaa kumuona Katibu wa itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi akiagiza mfanyabiashara wa mbolea feki akamatwe kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Mfanyabiashara huyo anatumia jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuuza Pembejeo feki na uwakala amepewa na Waziri Mkuu. Alidai mfanyabiashara huyo anatumia jina la Waziri mkuu.

Hili jambo haliwezi kuwa bahati mbaya hata kidogo kwa mfanyabiashara aliyeweka mtaji wake kutumia jina la kiongozi mkubwa wa nchi. Kuna uhusika waswali wanasema aliyekando haangukiwi na mti.

Mara kadhaa watu wa Kusini wamelalamika kuhusu kununua Pembejeo zisizokidhi viwango kutoka kwa hawa watu na Jamii inafahamu ukatili unaonafanywa Jeshi la Polisi lipo na Wakuu wa Ulinzi na usalama wapo wanajua ukweli wa hili sakata la Pembejeo feki nani ni muhusika Mkuu.

Mfanyabiashara gani mtwara mwenye nguvu ya Pesa kutumia jina la Waziri Mkuu kusambaza pembejeo feki, huu ni mchezo tunaochezewa.

Shaka ni mjumbe wa mjumbe wa kamati kuu ya CCM apeleke jina aliloambiwa ni muhusika Mkuu wa kuuza Pembejeo feki wanafanya uhalifu ulio wazi.

Kitendo cha mtu kuuza pembejeo feki ni cha uhujumu wa Kilimo na uchumi. Limetajwa jina la Waziri Mkuu kwenye Pembejeo feki achunguzwe.


Katibu Muenezi wa CCM akizungumzia dalali wa pembejeo bandia​
 
Tatizo letu viongozi wetu bado niwaoga au wanawadanganya wananchi, kama wana data zote kwanini wasiwatajie huyo mtu anayetumia hilo jina kama dhamana kwa wananchi
 
Tatizo letu viongozi wetu bado niwaoga au wanawadanganya wananchi, kama wana data zote kwanini wasiwatajie huyo mtu anayetumia hilo jina kama dhamana kwa wananchi

Tumeambiwa ni nguvu ya Pesa ni muhindi gani Mtwara mwenye ubavu huo wa kuuza pembejeo feki kwa jina la Waziri Mkuu.
 
Ama ni kweli au ndo "ukitaka kumuua paka, mpe jina baya"

Kwenye lile kundi, amebaki nani na nani kwani?
 
Kumekucha !

Eti mfanyabiashara kutumia jina la Waziri Mkuu au shaka ilibidi apunguze ukali wa maneno kuwa tetesi za Mtwara Waziri Mkuu anawauzia wakulima pembejeo feki kuzima moto shaka akatumtumia mfanyabiashara hewa asiyegusika anatumika kuuza mbolea feki Mtwara kwa jina la Waziri Mkuu.
 
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara,alitoa taarifa kuwa Mhusika amekwenda India kwa matibabu kwa mujibu wa mawakili wa mtuhumiwa.Ndiyo imetoka hiyo.
 
Kumekucha !
Ninahisi kuna vita kali inaendelea, ndani kwa ndani.

Huyu waziri mkuu wiki hii imekuwa ngumu sana kwake.

Mara aambiwe anatakiwa aoe mke wapili; mara anamhujumu rais na marafiki zake wafanya biashara kule bandarini.

Sasa tena yupo kwenye pembejeo feki?

Atapona huyu?
 
Nadhani Mama anatakiwa afanye maamuzi magumu alipofika sasa .....katelefoni ni pazito sana huruma nyingi mno .....usisahau ile Temeke kutumika kuvuruga ujenzi stand kwa faida ya waarabu na wapemba walio stand zao huko TMK.....uzuri eagle wanazo zote ...
 
Back
Top Bottom