Waziri mkuu kushindwa kukemea mawaziri inamaanisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu kushindwa kukemea mawaziri inamaanisha nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Escobar, Apr 12, 2012.

 1. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Muda huu naangalia bunge ambapo Mh. Freeman Mbowe kamuuliza Mh. Waziri mkuu kuwa kumekuwa na utaratibu wa mawaziri wa ccm wakiwa wanatumia magari ya serikali wanahudhuria kampeni na kuwatishia wananchi kuwa wakichagua upinzani serikali haitapeleka maendeleo kwenye maeneo yao na akatoa mfano ule wa kigoma mjini lakini pia Waziri Magufuli aliitumia kauli hiyo kule Igunga, Mary Nagu naye akatoa kauli hiyo kule Arumeru Mashariki lakini pia Naibu waziri wa ardhi akawaambia wananchi kuwa upinzani hauna serikali hivyo hauna msaada kwao na kamwe hautatatua matatizo yao. Swali likaja kwa waziri mkuu je, anawachukulia hatua gani mawaziri wanao tumia majukwaa kuwatishia wananchi na kuwalazimisha wachague kwa hofu ya kunyimwa huduma? Waziri mkuu akasema kuwa taratibu za kuongoza nchi zinatokana na katiba hivyo tufuate katiba.

  My take: Kuoneana haya kwa kisingizio cha kuwa kwenye mpambano wa kukifanya chama kishinde ndio kunawafanya mawaziri waseme chochote hata kama kinatafsiriwa kama rushwa ya uchaguzi. Mambo haya ndiyo yametufikisha kweye matusi ya kina Lusinde maana anajua hata akitukana still yuko safe ndani ya chama.
   
 2. n

  naroka Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Well said,kama upeo wao wa kufikiri ni huu wa Kibajaji,haishangazi kwa majibu hayo,na isitoshe PM kakwepa swali la msingi kitu ambacho kinaashiria hatari mbele yake na hofu kuu!!!
   
 3. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Natamani siku ya utawala wa Chadema viongozi wa awamu ya tatu na ya nne washuhudie utofauti wa uendeshaji wa dola na kuwaletea matumaini watz.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo huyo Pinda anakubaliana na huo uozo wa mawaziri wake kuwona wananchi mambumbu na kuwaadaha wananchi kwa kigezo cha mapambano ya vyama?what a ****!
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu punda bana, yeye anaona ni bora wafike hata kama watakuwa marehemu kuliko kuokoa wenzao wachache ili waje watoe ushuhuda wa namna ccm itakavyopotea
   
 6. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Wala sio habari za kushangaa tena hizo wana bodi.. Kwenye Mwananchi la leo kuna habari imeandikwa toka Serengeti.. Madiwani wa CCM wanapinga kwa nguvu zote Shule ilioyopo kwenye kata inayoongozwa na CDM kutopatiwa ufadhili wa Benki ya Dunia japo Shule ilikidhi vigezo vilivyotakiwa.. Na Madiwani walienda mbali zaidi na kutaka iundwe tume ya kwenda kumuona Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Kawambwa na Katibu mkuu wa CCM Wilson Mkama.. Madai yao ni kwamba kama Shule hiyo ikikarabatiwa then itawapa sifa CDM..!!
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Shame on them that's why we are here after 50yrs of independence.
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Nami nimeona, wakati nasubiri mwanangu mdogo amalize sikiliza Peoples power,kwani ndio shart nimepewa bila hivyo kilio siwezi kituliza.Mtoto wa Mkulima kwa pose kama kawa alibonyeza kitufe cha mic nikajua anamwacha Mbowe uchi kwa majibu safi.Ila alichojibu nilishtuka kidogo,Mbowe akasimama mpatia mifano km ushahidi jamaa akajibu kituko tena,nikaanguka katika sofa.Kwake kaona jamaa walikuwa ...vitani..na anasahau kuwa Lema naye alikuwa ..vitani...Soon yale majibu ya Pinda ya kufurahisha na ya akili yanatoweka kabisa, napengine ataangukia ktk udhaifu km ule aliounyesha ktk mgomo wa madaktari. Bora angelia tuu, tungelewa.serikali inakosa consistency +realibility ktk mambo yake.

  Msishangae viongozi wengi wa serikali wakjikuta ktk muda mfupi wanahitajika kwa mstaafu ocampo kujibu mashitaka.Wana majibu mepesi sana, wana kauli zisizo makini, na wanajitokeza kirahisi ktk matukio mabaya just because ni chama chao.

  Wengine inabidi wajifunze jitenga na mambo hatarishi yanayofanywa na watendaji wa serikali,kwani yatawahukumu mara tuu ukatili dhidi ya raia utakaposhika macho ya hawa jamaa wa mahkama ya kimataifa.Sijui km serikali yetu ina mikataba ya kuwapa kinga mawaziri , wabunge, na police km walivyo askari na viongozi wa marekani.So wasijisahau sana ktk mambo ya ushabiki.
   
 9. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Tanzania, tanzania, nakupenda kwa moyo woteeeee, nchi yangu tanzania, jina lako ni tamu sanaaaaaaa!
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kiongozi goi goi hawezi kumkemea mwenzake... We want mtu kama Raila Odinga ambaye anakuw ahaogopi hata Rais anamzingua tu kama akikosea..
   
 11. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pinda ananikumbusha ile statement maarufu ya Mh. Kapwepwe RIP kwa uingereza miaka ile aliposema "Britain is a toothless dog wagging its tail before Ian Smith". Ilileta utata sana lakini ujumbe ulifika. Mtoto wa mkulima is toothless hivyo tusitegemee maajabu toka kwake bali rhetorics.
   
 12. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  CCM wana upofu wa akili
   
 13. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I don't expect anything good from Hon. Pinda; The guy can talk.. but no action so far.....You better don't give him a chance to talk to you.
   
 14. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jibu ni walichofanya mawaziri sio sahihi but hakuwa muwazi kukiri hivyo that is why kasema mawaziri wanaongozwa na katiba na katiba haibagui kwa misingi ya siasa...........nlitegemea jibu la namna hiyo ktk mfumo gamba wa kulindana!!!!!!!!
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  The statement you quoted was not made by the late Simon Kapwepwe but by Ali Simbule another vibrant UNIP MP from northern Zambia!! I stand to be corrected.
   
Loading...