Waziri Mkuu: Kuna uwezekano Mkubwa Taifa Stars kufuzu kuingia Kombe la Dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Watanzania wanatamani kuona timu zao za Taifa za michezo mbalimbali zikifanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo, Novemba Mosi, 2021 wakati wa kikao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa , uongozi wa TFF pamoja na wadau wa mpira wa miguu kilichofanyika ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

Amesemaa uwezekano wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni mkubwa kutokana na matokeo mazuri ambayo imeyapata katika michezo yake minne ya awali.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewataka Watanzania na wadau mbalimbali wa soka nchini kuunganisha nguvu kuisaidia timu ya Taifa Stars ili ifanya vizuri katika mechi zilizobaki za kufuzu kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia.

“Itakuwa ni jambo jema sana tukiwa tunasherehekea miaka 60 ya Uhuru, pia tukashereheka kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia timu ya Taifa kufuzu kucheza kombe la duani nchini Qatar” Amesema Waziri Bashungwa.
 
Hongera sana Serikali ya awamu ya Tano kwa mazingira wezeshi yaliyopelekea kupatikana ya Sita ambayo inawezesha haya
 
Watz shida yetu ni kwamba hatujiamini na kupenda kubeza
Unaanzaje kujiamini, wachezaji wenyewe wako wapi? Nchi inawaza kwenda kombe la dunia lakini ndani ya hiyo nchi kuna klabu imeshindwa kushiriki mashindano ya kimataifa kwa sababu ambazo sio za kimichezo. Sasa wachezaji wazoefu angalau watatoka wapi? Kiufupi ni kwamba tunategemea bahati zaidi kuliko uwezo maana hatua ya knock out tutakapokutanishwa na Algeria au Nigeria, Egypt, Tunisia, Morocco, Ghana,Senegal n.k ni bahati tu inayotegemewa kwamba itatuvusha.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Watanzania wanatamani kuona timu zao za Taifa za michezo mbalimbali zikifanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo, Novemba Mosi, 2021 wakati wa kikao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa , uongozi wa TFF pamoja na wadau wa mpira wa miguu kilichofanyika ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

Amesemaa uwezekano wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni mkubwa kutokana na matokeo mazuri ambayo imeyapata katika michezo yake minne ya awali.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewataka Watanzania na wadau mbalimbali wa soka nchini kuunganisha nguvu kuisaidia timu ya Taifa Stars ili ifanya vizuri katika mechi zilizobaki za kufuzu kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia.

“Itakuwa ni jambo jema sana tukiwa tunasherehekea miaka 60 ya Uhuru, pia tukashereheka kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia timu ya Taifa kufuzu kucheza kombe la duani nchini Qatar” Amesema Waziri Bashungwa.
Labda Mwijaku apewe dhima ya kuhamasisha. Huyo ndo anaweza.
 
Hivi team za kombe la Dunia kwa Africa mwaka 2022 zinaongezeka?Toka tano kwenda mbele

Maana Ghana Naigeria Cameroon ivory Coast Algeria Tunisia Egypt ndio wanaopaswa kutuwakilisha kidogo mali
 
Back
Top Bottom