Waziri Mkuu kuanza ziara ya siku nne Kigoma leo

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
500
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuanza ziara ya kiserikali ya siku nne mkoani Kigoma leo kuimarisha zao la michikichi kama moja ya mazao makuu ya kibiashara kwa kulipa kipaumbele zaidi. Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga aliwaambia waandishi wa habari jana katika siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma, Waziri Mkuu pamoja na kupata taarifa ya mkoa, pia atakutana na kufanya mazungumzo na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika osi za chama hicho mjini.

Maganga alisema katika siku ya pili ya ziara yake, Waziri Mkuu atatembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kihinga Wilaya ya Kigoma kukagua uzalishaji wa miche ya michikichi kutekeleza agizo alilolitoa katika ziara yake ya kiserikali mwaka jana Kigoma kuhakikisha wakulima wanapata mbegu za kutosha. Mkuu huyo alisema baada ya kutoka Kihinga, Waziri Mkuu atatembelea Gereza la Kwitanga Kigoma Vijijini kukagua shamba la michikichi na kuzindua trekta litakalotumika kwa kilimo cha michikichi, kazi kama hiyo pia itafanyika kwenye Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Bulombora Wilaya ya Kigoma.

RC Maganga alisema katika siku ya tatu, Waziri Mkuu, Majaliwa atatembelea Kijiji cha Mwamila Wilaya ya Uvinza kukagua kitalu cha miche ya michikichi na baadaye kuongoza kazi ya upandaji miti kando kando ya barabara katika eneo la Lugufu Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Uvinza. Akielezea kuhusu kilimo cha michikichi, Maganga alisema maagizo ya Waziri Mkuu kufanya mchikikichi kuwa moja ya mazao makuu ya biashara nchini na Kigoma moja ya mikoa inayozalisha mafuta ya mawese kwa wingi, yameanza kutekelezwa na kinachofanywa ni ukaguzi kuona utekelezaji wa maagizo hayo.

Aidha, Waziri Mkuu atatembelea Wilaya ya Kibondo ambako atazuru Kambi ya Wakimbizi wa Burundi ya Nduta na soko la mpakani linalotumiwa na Watanzania na raia wa Burundi katika Kijiji cha Mkarazi. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, Maganga, Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake wilayani Kakonko Februari 19, mwaka huu kwa kuweka jiwe la msingi la Osi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na baadaye kuzungumza na wananchi katika stendi ya mabasi mjini Kakonko. Baada ya mkutano huo, Waziri Mkuu ataondoka kwenda Kagera kwa ziara nyingine ya kiserikali.
 
Bensonpeace

JF-Expert Member
Jun 2, 2017
490

Kigoma sio sehemu ya Tanganyika/Tanzania nakumbukuka tu huu msemo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom