Waziri mkuu Kassimu Majaliwa ajiandikisha kupiga kura na kuonya vikali upotoshaji

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
OKTOBA 13, 2019

Kutokea Ruangwa Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amejiandikisha katika daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Majaliwa na Mkewe, Mary Majaliwa wamejiandikisha leo Jumamosi Oktoba 12,2019 katika kituo cha shule ya msingi Nandagala, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuhamasisha kujitokeza kwa wingi na kupuuza upotoshaji wa kadi za uchaguzi mkuu kwamba zitatumia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Miongoni mwa sifa za mtu anayetakiwa kujiandikisha kwa ajili ya kuchagua kiongozi ngazi ya Kijiji, Kitongoji au mtaa kupitia uchaguzi huo ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, mwenye umri miaka 18 au zaidi, awe na akili timamu.

Pamoja na sifa hizo, mgombea atalazimika kuwa na umri unaoanzia miaka 21 au zaidi na awe raia mwenye shughuli ya kujipatia kipato.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Mkuu amesema shughuli ya kujiandikisha ni ya kitaifa inayowezesha kuchagua kiongozi umtakaye au kugombea katika uchaguzi huo.
 
Attachments

  • pic+majaliwa.gif
    pic+majaliwa.gif
    107.2 KB · Views: 1

TUTAAMINI VIPI KAMA AMEJIANDIKISHA WAKATI HANA KITAMBULISHI CHOCHOTE?
 
Back
Top Bottom