Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,961
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

 
Sasa serikali hapa ndio wanaonyesha kupoteana, ilitakiwa kama waliamua kukaa kimya basi wangekaa kimya wala wasishindane na watu wa mitandaoni.

Ila kwa hili la kuanza kumjibia Mh. Rais watu wataanza kuunganisha doti. Cha msingi waendelee kukaka kimya huku wakitimiza majukumu yao ya kila siku.
 
75 Reactions
Reply
Back
Top Bottom