Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutumia takwimu ambazo siyo rasmi hajavunja Sheria?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,657
22,252
Sheria ya takwimu iliyopitishwa hivi karibuni inakataza matumizi na kutangaza takwimu zisizo rasmi, nimemsikia Waziri Mkuu akiijulisha dunia kuwa watu bilioni 3.9 wamefuatilia msiba wa Hayati JPM. Takwimu hizo bahati mbaya siyo rasmi ila kwake zimemfurahisha kwani ni ushindi.

Huko nyuma tumewahi kushuhudia mtu akiweka takwimu zilizonona Serikali huzikubali licha kisheria ni batili, lakini MTU huyo huyo atakapotoa takwimu zilizokondeana kufuata na wakati hutafutwa akamatwe.

Je, Waziri Mkuu anapotumia takwimu zisizo rasmi ni sahihi au kosa kisheria?

Pia soma > Waziri Mkuu: Watu Bilioni 3.9 Duniani jana walifuatilia Shughuli za Kumuaga Hayati Magufuli
 
Unaumiza kichwa kwa mtu muongo! Ngoja tuone baada ya mazishi kama ataendelea kubebwa, au atawekwa pembeni.

Maana ameshapoteza mvuto kitambo sana. Kuanzia uongo wake wa ajira 5000 za walimu kule Bungeni, Mzee anapiga kazi kama kawaida, nk.
 
Mods naomba muondoe jina Kassim Majaliwa, Mimi ninazungumzia cheo (wadhifa) si mtu.
 
Hata kama amedanganya, tukiweka chuki pembeni ni kweli maziko ya jiwe yanafuatiliwa sana kwa sababu sio alikuwa anapendwa, ni kwamba watu hawakutegemea atakufa, alafu kwamba alikuwa mgonjwa wa moyo hilo limeniumiza hata mimi binafsi.
 
Hata kama amedanganya, tukiweka chuki pembeni ni kweli maziko ya jiwe yanafuatiliwa sana kwa sababu sio alikuwa anapendwa, ni kwamba watu hawakutegemea atakufa, alafu kwamba alikuwa mgonjwa wa moyo hilo limeniumiza hata mimi binafsi.
Maziko yanahusiana vipi na sheria ya takwimu, sheria husimama kama ilivyo haifuati jua au mvua, giza au mbaramwezi, msiba au harusi, sheria ni sheria.
Tujadili kuhusu sheria ya takwimu tu.
 
Maziko yanahusiana vipi na sheria ya takwimu, sheria husimama kama ilivyo haifuati jua au mvua, giza au mbaramwezi, msiba au harusi, sheria ni sheria.
Tujadili kuhusu sheria ya takwimu tu.
Mkuu hivi unategemea kweli kabisa kwamba hao jamaa huwa wanaangalia sheria kwenye kufanya chochote? , siku ya kwanza tuu walikosea kutaja siku za Maombolezo kisheria, kimsingi ni kuangalia point of fact, katika point of law wanakosea mengi mnoo.
 
Kwanini baadhi ya watu hapa wanaonesha chuki binafsi kwa PM Majaliwa Majaliwa?

Jueni kuwa the guys is smart kichwani. JPM moja ya sifa zake alijitahidi sana kuzungukwa na Watu makini wakati wote. Na ndio maana hata Dr Bashiru alichomoza baada ya mafisadi wa kiongozwa na mkuu wao kutaka kumzibia.

Hivi kama wewe si mnafiki unawezaje kusifia mafanikio ya JPM na kumpa heshima JPM ushindwe kuelewa PM ndiye kiranja mkuu wa Baraza la mawaziri la JPM?

Hivi unaweza kuona kukubalika huku kwa JPM na waombolezaji kulikovunja rekodi pengine tangu kuumbwa kwa Tanzania halafu ukutenge na Rais SSH, PM na watendaji wengine walio fanya kazi na JPM!?

Naomba mtu mwenye makarama na hikma ya Mungu wa Mbinguni aniambie hii kibwagizo inayo shika kasi ya moto wa nyikani ya waombolezaji wanao sindikiza mwili wa almaruhum JPM, Kibwagizo JPM/Magufuli -Jeshi inatoa ujumbe gani?
 
Yule siku hizi hana utofauti na kasuku,yaani,anaropoka ropoka. Nahisi ni kutokana na kutojua hatma yake. Watu wa Tunduru hawatamsahau kwa kuwaletea kituko chake ambacho ndio mbunge wa Tunduru kaskazini. Alaaniwe daima.
 
Mtu anakuambia eti Majaliwa yuko smart kichwani, Majaliwa hana u smart wowote kichwani. Mtu anayedanganya umma ndani ya nyumba ya ibada, ana u smart gani?
 
Back
Top Bottom