Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukutana na kuongea na Vyama vya Siasa Oktoba 21 - 23

Lengo la mkutano huo ni kuzungumzia namna ya kufanya shuguli za kisiasa.

Bbc wamesema vyama vya upinzani kukutana na Waziri Mkuu.

Kwenye mkutano wa awali ulioitishwa na msajili Mtungi, CHADEMA na ACT Wazalendo walikataa kufika wakidai Mtungi na polisi ndio wanaovibana vyama vyao. Walihitaji uwepo wa Waziri Mkuu na mawaziri wenye dhamana ili mkutano uwe na tija.

Naona Serikali kupitia Waziri Mkuu wametekeleza hilo ili kuwe na muafaka Kama taifa.

Kwa uwepo wa Waziri Mkuu na Mawaziri wengine wenye dhamana na bila kutaja uwepo wa Sirro.

Nadhani CHADEMA na ACT pia watakuwepo. Na kubwa zaidi mkutano huo umetangazwa na makamu msajili na sio Jaji Mtungi ambaye CHADEMA na ACT hawaoneshi kumuamini.

Swali ninalojiuliza.
Je, kwanini Rais hakutimiza ahadi ya kukutana na kuongea na CHADEMA tokea Aprili 20 aliyoitoa kwa Mbowe.

Kwanini washauri wa Rais hawakutaka kabisa Mbowe na Rais Samia wakutane. Hata Kama Mbowe ni mwongo walikuwa na nafasi ya kushauriana na Rais baada ya kuongea na Mbowe.

Je, mkutano huo utakuwa na nguvu kiasi gani wakati kiongozi mkubwa zaidi wa upinzani yuko Mahabusu kwa kesi isiyodhaminika.

Je, Kuna maafikiano ya haki yanayoweza kupatikana wakati Wabunge 19 wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama bado wako bungeni?

Je, wewe kama Mtanzania unashauri upinzani ukaongelee nini haswa.
Namna ya kufanya siasa hakujadiliwi na raisi,waziri mkuu, msajili Wala yeyote yule. Katiba yetu (ingawa Ina mapungufu ya msingi) imeweka taratibu za kufanya, siasa wao Kama wameamua kufanya uvunjaji wa sheria kwa kutumia polisi waendelee
HAKUNA sababu ya kukutana na watu hao hao wasiokemea hata huu uvunjaji wa sheria ikiwa wao Ni wanufaika no 1.
Labda Kama Ni kuweka kumbukumbu sawa
 
Wakutane ili kufanya talks of the talks! Hata kama wanaamini si right person but nikujiweka in the position of strength
 
CHADEMA, iwe ni marufuku kushiriki mkutano wowote na hawa watu waliombambikizia kesi Mbowe, mpaka watakapofuta mashtaka yao hewa.
 
Tunahitaji Amir Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanz na Mwenyekiti wa Chama kilichounda Serikali. Vinginevyo ni danganya toto.
Nazani wahudhurie tu. Kwa siku 3 wanavitu vingi vya kujadili. Lazma wawe na maazimio yenye muda maalumu wa kutekeleza.
 
Lengo la mkutano huo ni kuzungumzia namna ya kufanya shuguli za kisiasa.

Bbc wamesema vyama vya upinzani kukutana na Waziri Mkuu.

Kwenye mkutano wa awali ulioitishwa na msajili Mtungi, CHADEMA na ACT Wazalendo walikataa kufika wakidai Mtungi na polisi ndio wanaovibana vyama vyao. Walihitaji uwepo wa Waziri Mkuu na mawaziri wenye dhamana ili mkutano uwe na tija.

Naona Serikali kupitia Waziri Mkuu wametekeleza hilo ili kuwe na muafaka Kama taifa.

Kwa uwepo wa Waziri Mkuu na Mawaziri wengine wenye dhamana na bila kutaja uwepo wa Sirro.

Nadhani CHADEMA na ACT pia watakuwepo. Na kubwa zaidi mkutano huo umetangazwa na makamu msajili na sio Jaji Mtungi ambaye CHADEMA na ACT hawaoneshi kumuamini.

Swali ninalojiuliza.
Je, kwanini Rais hakutimiza ahadi ya kukutana na kuongea na CHADEMA tokea Aprili 20 aliyoitoa kwa Mbowe.

Kwanini washauri wa Rais hawakutaka kabisa Mbowe na Rais Samia wakutane. Hata Kama Mbowe ni mwongo walikuwa na nafasi ya kushauriana na Rais baada ya kuongea na Mbowe.

Je, mkutano huo utakuwa na nguvu kiasi gani wakati kiongozi mkubwa zaidi wa upinzani yuko Mahabusu kwa kesi isiyodhaminika.

Je, Kuna maafikiano ya haki yanayoweza kupatikana wakati Wabunge 19 wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama bado wako bungeni?

Je, wewe kama Mtanzania unashauri upinzani ukaongelee nini haswa.
Katiba ndio inayoelekeza namna gani shughuli za kisiasa zifanyike,sio waziri mkuu.

Labda wakutane kusisitiza katiba ifuatwe sio kujadili vinginevyo.
 
Waziri Mkuu kama Majaliwa hana Mamlaka yoyote ya kisheria ya kukutana na vyama vya siasa .

Bila shaka Chadema haitahudhuria jambo hilo
Unasahau kuna wanachama 19 +1 wa Chadema ambao wakati wowote wakihitajika wanawakilisha chama chao? "Chadema " watawakilishwa tu, wapende wasipende. Kama vile wanavyowakilishwa bungeni.

Amandla...
 
Unachomoa gurudumu la gari la jirani yako halafu, badala ya kurudisha hilo gurudumu, unamuita azungumze na mdogo au mtoto wako ili “muafaka” wa “tatizo” upatikane!

Bila shaka serikali hii inaamini kwa dhati kabisa kuwa watu inaowangoza ni mazuzu. Ukweli ni kuwa hawataki serious opposition kabisa.
Hawa wamejiweka madarakani, wewe utafanyaje? Na wale darasa la saba walinzi wa benk, wanapiga sana kama mwizi! Utafanyaje?
 
Shughuli za Kisiasa halali zilizo ainishwa kwenye Katiba limekuwa jambo la kuomba Kha!
CCM wapuuzi sana Shwain!
oday2.png
 
Back
Top Bottom