William Mshumbusi
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,657
- 2,252
Lengo la mkutano huo ni kuzungumzia namna ya kufanya shuguli za kisiasa.
Bbc wamesema vyama vya upinzani kukutana na Waziri Mkuu.
Kwenye mkutano wa awali ulioitishwa na msajili Mtungi, CHADEMA na ACT Wazalendo walikataa kufika wakidai Mtungi na polisi ndio wanaovibana vyama vyao. Walihitaji uwepo wa Waziri Mkuu na mawaziri wenye dhamana ili mkutano uwe na tija.
Naona Serikali kupitia Waziri Mkuu wametekeleza hilo ili kuwe na muafaka Kama taifa.
Kwa uwepo wa Waziri Mkuu na Mawaziri wengine wenye dhamana na bila kutaja uwepo wa Sirro.
Nadhani CHADEMA na ACT pia watakuwepo. Na kubwa zaidi mkutano huo umetangazwa na makamu msajili na sio Jaji Mtungi ambaye CHADEMA na ACT hawaoneshi kumuamini.
Swali ninalojiuliza.
Je, kwanini Rais hakutimiza ahadi ya kukutana na kuongea na CHADEMA tokea Aprili 20 aliyoitoa kwa Mbowe.
Kwanini washauri wa Rais hawakutaka kabisa Mbowe na Rais Samia wakutane. Hata Kama Mbowe ni mwongo walikuwa na nafasi ya kushauriana na Rais baada ya kuongea na Mbowe.
Je, mkutano huo utakuwa na nguvu kiasi gani wakati kiongozi mkubwa zaidi wa upinzani yuko Mahabusu kwa kesi isiyodhaminika.
Je, Kuna maafikiano ya haki yanayoweza kupatikana wakati Wabunge 19 wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama bado wako bungeni?
Je, wewe kama Mtanzania unashauri upinzani ukaongelee nini haswa.