Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Karibu Mwanza karibu kituo cha polisi Kirumba

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,096
1,332
Kama kweli serikali ya awamu ya 5 imeamua kutumbua majipu, Kwa hapa mwanza kaeibuni kirumba polisi, wanamsemo wao mmoja kuingia bure kutoka hela. Oc Cid Kim, inspector Swalehe pamoja na viongozi wengine wamekua wanawapangia vijana wao doria usiku wakitumia mafuta ya serikali kuzungukia vijiwe vya wauza mirungi, akina pesa, saba, mama azzaa, mmeru na wengineo hapa mwanza mjini wakichukua kama kodi vile, pia kuna maskari polisi wamekua wakizunguka Kwa wauza mirungi na kuchukua mirungi kwajili ya matumizi yao wanajulikana, na mbaya zaidi wamekua wakiwakamata wala mirungi na kuwaweka ndani huku wakiwapa vitisho vya hapa na pale halafu inapotakiwa dhamana huomba pesa kuanzia laki 5 ili mambo yaishie hapohapo, wamejisahau sana wanadharau wanajiamini kupita kiasi wanachukuarushwa hadharani akina Afande barikiwa, deo, na wengineo hawana aibu kumuomba rushwa mtuhumiwa yoyote, hali ndani ya selo zao ni mbaya sana kuna watu wenye kesi siziso na kichwa wala miguu lakini huwekwa humo ndani hadi mwezi imefikia hatua askari anakwambia tafuta hata elf5 utoke, Bila hivyo hutoki na mahakamani huendi.

Kwa ujumla kuna mengi kuhusiana na kituo hicho pia na ushahidi upo hadi Wa picha na masauti.
tutumbulieni hill jipu ili wananchi tuzidi kuiamini serikali yetu.

karibu sana waziri mkuu , Tunaimani na serikali yako ya awamu ya 5.
 
Mkuu
Nikupongeze kwa kulisema jambo hili kiduchu katika matatizo mengi yanayowakwaza raia kwa jeshi la polisi. Nikupongeze pia kwa uamuzi wako wa kwenda mbele na kuanika majina ya wanaohusika. Ni Mwanzo mzuri kwamba raia wanafika mahali wanaeleza kile kinachowakwaza katika kupatiwa huduma!

Hata hivyo, kama sio majungu ingekuwa vyema wakati mwingine twende mbele tuseme askari xy, jumatano ya tarehe.... saa .. katika eneo la ..... alifanya hivi na vile ili pamoja na mambo mengine itawasaidia sio tu wachua hatua bali wanaofanya vitedo hivyo kubaini kuwa sasa wananchi wanaweza kueleza juu ya kile wanachokifanya.

Inawezekana kabisa hiyo ndio cghangamoto unayotaka huyo mzee wa kutumbua majipu aifanyie kazi, lakini binafsi ningependa amuangalie mkuu wa mkoa wa Mwanza. Zile gharama alizotumia kuishi hotelini kwa miezi zaidi ya mitatu yeye na familia yake, atazirudisha?.
 
Safi sana mtoa mada, hv ndio inatupasa watanzania tuwe.tumsaidie dokta na timu yake kusafisha nchi kwa kufichua maovu.lkn cyo tuwe watu wa kulalamika kila cku
 
Mamluki wakiTanzania wanaishi kwa madhila na uonevu 24/7 !!! Ukiwa mnyonge na masikini utabambikiziwa kesi !!
 
hii ndo democracy

africa ;Tanzania tunatisha; ukopeshi, unapiga pekupeku............dahhhhhhhhhhhh
Umungunyi ata maneno.
ATA KITUO CHA POST YOMBO VITUKA; TEMEKE ;
UKIKAMATWA ; KUTOKA ELFU 5000- 20000
 
Wewe lazima muuza mirungi. Katika wilaya zenye amani na utulivu Tanzania na matukio machache ya wizi na ujambazi ni Ilemela. Kuna mitaa tunalala milango wazi.

We dawa achana na kula mirungi na sio kuchochea wakamataji wahamishwe
 
Hv huyu mkuu wa mkoa wa mwanza atatumbuliwa lini?
Sio huyo tu, kuna mkurugenzi wa Ilemela alitumbuliwa na Jaffo akarudishwa na Simbachawene amehamisha wafanyakazi nane wa idara ya fedha na manunuzi kwa kuhofia watamzibia kwenye wizi. Haiyumkiniki kuwa na serikali inadai inapambana na ufisadi huku wafanyakazi wasio mafisadi wananyanyaswa na mkurugenzi fisadi. Wahasibu watano wamepelekwa kuwa wahasibu na shule za kata. Majaliwa ufike na pale
 
Kama kweli serikali ya awamu ya 5 imeamua kutumbua majipu, Kwa hapa mwanza kaeibuni kirumba polisi, wanamsemo wao mmoja kuingia bure kutoka hela. Oc Cid Kim, inspector Swalehe pamoja na viongozi wengine wamekua wanawapangia vijana wao doria usiku wakitumia mafuta ya serikali kuzungukia vijiwe vya wauza mirungi, akina pesa, saba, mama azzaa, mmeru na wengineo hapa mwanza mjini wakichukua kama kodi vile, pia kuna maskari polisi wamekua wakizunguka Kwa wauza mirungi na kuchukua mirungi kwajili ya matumizi yao wanajulikana, na mbaya zaidi wamekua wakiwakamata wala mirungi na kuwaweka ndani huku wakiwapa vitisho vya hapa na pale halafu inapotakiwa dhamana huomba pesa kuanzia laki 5 ili mambo yaishie hapohapo, wamejisahau sana wanadharau wanajiamini kupita kiasi wanachukuarushwa hadharani akina Afande barikiwa, deo, na wengineo hawana aibu kumuomba rushwa mtuhumiwa yoyote, hali ndani ya selo zao ni mbaya sana kuna watu wenye kesi siziso na kichwa wala miguu lakini huwekwa humo ndani hadi mwezi imefikia hatua askari anakwambia tafuta hata elf5 utoke, Bila hivyo hutoki na mahakamani huendi.

Kwa ujumla kuna mengi kuhusiana na kituo hicho pia na ushahidi upo hadi Wa picha na masauti.
tutumbulieni hill jipu ili wananchi tuzidi kuiamini serikali yetu.

karibu sana waziri mkuu , Tunaimani na serikali yako ya awamu ya 5.
We nawe ni teja.
 
Back
Top Bottom