Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka watanzania waishio Canada wawe na uzalendo kwa Taifa lao

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
ac6b46606c1744f3db33d4542d3b628b.jpg
26bbd17274c1fde1cfe923b1e0e0bcbe.jpg
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.

Ametoa wito huo jana Oktoba 31, 2017 wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.

Waziri Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake.

"Tembea huku ukiringia nchi yako, wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, iseme vizuri kama ambavyo wengine wanasema vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo".

Aliwataka wakumbuke kuweka akiba na wanapopata fursa watume fedha zao nyumbani ili zisaidie kuleta maendeleo.

"Ukipata kitu kidogo, rusha nyumbani, ukimpata mtu anayeweza kuleta tija, mlete nyumbani, nasi tutawapokea wewe na yeye", alisisitiza.

"Tunawasisitiza muitangaze nchi yenu kwa mataifa mengine ili nao waone kuwa Tanzania ni mahala pa fursa, na akitaka kuwekeza ajue kuwa anawekeza mahala ambapo ni salama", alisema Waziri Mkuu.
 
Tanzania haina mazingira rafiki kwa wawekezaji, na Magufuli ni rais msema ovyo anaharibu sifa ya nchi nje wawekezaji hawataki kuja.

Waziri Mkuu anajua haya?
 
Huyo waziri mkuu ameshindwa kuujenga huo uzalendo kwa watanzania waliopo hapa hapa Tanzania, atawezaje kuujenga huo uzalendo kwa walowezi wa kitanzania waliokimbia msoto wa maisha hapa Tanzania na kwenda kuishi Canada?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom