Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka HESLB kurekebisha baadhi ya dosari utoaji mikopo kwa wanafunzi

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutafakari namna ya kurekebisha baadhi ya dosari zilizopo likiwemo suala la kuwanyima mikopo wanafunzi kwa kutumia kigezo cha kusoma katika shule binafsi. Amesema kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamefaulu vizuri kidato cha nne na wamekosa nafasi katika shule za Serikali na wanatoka katika familia zisizokuwa na uwezo, hivyo wanatafuta wafadhili ambao wanawasomesha kwenye shule binafsi
.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Agosti 10, 2019) wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Amesema kitendo cha bodi hiyo kuwanyima mikopo baadhi ya wanafunzi kwa kigezo cha kusoma katika shule binafsi bila ya kujiridhisha kama wanatoka kwenye familia zenye uwezo au zisizokuwa na uwezo kinawanyima wanafunzi hao fursa za kuendelea na masomo. Pia ametumia fursa hiyo kuwaonya wakuu wa vyuo vikuu ambao wanatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi kwa kuzipeleka katika miradi mbalimbali baada ya kuzipokea kutoka HESLB na kuwacheleweshea wanafunzi stahiki yao.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa vyuo vikuu kuimarisha mafunzo kwa njia ya vitendo kwani tafiti nyingi zinazohusu mambo ya ajira zimebainisha umuhimu wa mafunzo ya vitendo katika kumuwezesha mhitimu kuwa na uelewa na ujuzi mpana wa kile alichokisoma kwa njia ya nadharia. “Vyuo viongeze umakini na ufuatiliaji wa karibu wa vijana wetu wanapokuwa kwenye elimu kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba wanapata maarifa na ujuzi uliokusudiwa katika mitaala yao. Pia natoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi watoe ushirikiano wa dhati kwa wanafunzi wanaotafuta nafasi za kufanya mafunzo kwa njia ya vitendo kwenye taasisi zao.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAHLISO, Bw. Peter Niboye amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu ni ucheleweshwaji wa mikopo kwa baadhi ya vyuo licha ya HESLB kuwasilisha fedha hizo mapema, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo. Kadhalika, Mwenyekiti huyo wa TAHLISO, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ushirikiano mkubwa inaoipatia jumuiya hiyo hivyo kurahisisha utendaji wake.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Patrobas Katambi alimkabidhi Waziri Mkuu hati ya kiwanja kilichoko katika eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TAHLISO, ambapo baada ya kupokea hati hiyo, Waziri Mkuu aliikabidhi kwa Mkwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw. Niboye.

Mkutano huo umehudhuriwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Godfrey Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori pamoja na viongozi kutoka vyuo mbalimbali nchini vinavyounda TAHLISO.
 
Aah jaman hawa Bodi ni basi tu hamna alternatives za kukopa iyo fedha mahala pengine

Hawa jamaa deni lao linakuwa( kimo na umbo na umri) kitu ambacho hata benk za biashara huwa deni halikuwi

Wana terminology moja iyo inaitwa 'rentation fee' hiyo kitu ni kichaka cha kuongeza deni la wateja wao

Nashawishika kama nina uwezo ni Bora nisomeshe mwanangu kwa gharama zangu

Deni tunakutana nalo mpaka u kasema Bora ya Benk za Biashara ila sio hao

HESLB ni mziki mwingine
 
Hizo ni kauli za kisiasa tu. Bodi imeweka wazi kabisa kama ulisoma shule binafsi kwa ufadhili uonyeshe ushahidi. Sasa ushahidi huna alafu unawalaumu bodi?

Pili hili la kupenda kukopa kopa ni ujinga tu, mtu amesoma shule ada milioni 5 unashindwaje kulipa ada ya chuo ambayo kwa hapa Tanzania haizidi 2M kwa mwaka na hata mkopo hawakupi hela ya chakula inayozidi 4M kwa mwaka.

Ukiweza achana na huo mkopo kabisa. Leo waliokopa huko nyuma wanatamani hata wasingefanya hivyo.

Kopa tu kama una uhitaji huo mkopo. Kama una uwezo jilipie masomo.
 
Hii bodi Ni jipu.kwa mtazamo wangu bodi ingetoa mikopo kwa wote walioomba maana Ni mkopo sio hisani.
 
Leo tarehe 11 Deember, 2019 siku ya jumapili, nikiwa nasikiliza Redio Free Africa katika kipindi cha Matukio, nmesikia habari ikisema waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh Khasim Maliwa Majaliwa amesema mikopo ya elimu ya juu itolewe kwa wanafunzi wote hata waliosoma shule za binafsi (Private)!
Nilitamani kurewind habari nikagundua sisikikizi CD,Flush wala cassete kwa hiyo habari ikawa imepita hivyo sikuweza kusikia alisema akiwa wapi lakini naamini ni redio inasikiluzwa na watu wengi na nina uhakika ni wengi wamesikia hiyo taarifa.
Kilichonifanya nitamai kurewind ni maswali kibao yaliyoingia kichwani mwangu.
1. Hili limetoka kwa sababu 2020 hata wakiokuwa wananyimwa hiyo mikopo kwa vile wamesoma shule binafsi watahitajika?

2. Kuna ziada ya pesa imepatikana hivyo na wale waliokuwa wananyimwa hata ufaulu wao ni wa daraja la kwanza wapewe?

3. Wanafunzi wanaojiunga na vyuo toka shule za serikali wamepungua hivyo pesa zingine wapewe waliosoma shule binafsi?

Maswali hayo yameniijia sababu miaka mitaty iliyopita yaani waliojiunga n vyuo mwaka 2016 wanajua kilichowapata. Waliokuwa wamesoma shule binafsi walibaguliwa utafikiri hawakuwa watanzania na utafikiri wazazi wao hawalipi kodi. Walinyimwa mikopo hata kama wameoata daraja la kwanza kwa maana ya kuwa wazazi wao wana uwezo! Serikali haikutaka hata kufikilia wengine walisoma kwa hisani za watu baki,serikali haikutaka hata kufikilia kuwa hao watoto yamkini wazazi walishafilisika. Hawakusikilizwa hata kama wazazi waliuza hadi mashamba ili watoto wao wapete elimu itakayowafanya wafaulu vizuri kidato cha sita wapate daraja la kwanza iki wasomeshwe kwa mikopo!
Serikali iliwatolea maneno makali! Kwa nini serikali ikopeshe watoto wa wazazi wenye uwezo?
Serikali haikutaka hata kujiuliza kuwa kuna matajiri wakubwa na wanasomesha watoto wao shule za serikali! Hawakusikilizwa!!
Leo kuna kitu gani hadi mtendaji mkuu aseme wanafunzi waliosoma shule binafsi nao wakopeshwe? Ili iweje? Au ndo ushawishi wa 2020?
Kwa nini msimamo usiwe ule ule wa kutowakopesha waliosoma shule binafsi na tamko hili basi lije baada ya 2020?
Serikali hata haisemi imeamua hivyo kwa sababu gani maana iliwanyima kwa sababu.

Kweli yajayo yanafurahisha.
 
Jiulize kwanza zile milioni 50 kila kijiji zilishatolewa? Utapata jibu
 
Hizo ni kauli za kisiasa tu. Bodi imeweka wazi kabisa kama ulisoma shule binafsi kwa ufadhili uonyeshe ushahidi. Sasa ushahidi huna alafu unawalaumu bodi?

Pili hili la kupenda kukopa kopa ni ujinga tu, mtu amesoma shule ada milioni 5 unashindwaje kulipa ada ya chuo ambayo kwa hapa Tanzania haizidi 2M kwa mwaka na hata mkopo hawakupi hela ya chakula inayozidi 4M kwa mwaka.

Ukiweza achana na huo mkopo kabisa. Leo waliokopa huko nyuma wanatamani hata wasingefanya hivyo.

Kopa tu kama una uhitaji huo mkopo. Kama una uwezo jilipie masomo.
Unaongea hivyo sababu kwenu pesa ipo na kama haipo familia nzima iliishia ka saba na kidato cha nne hivyo unaona wengi mkose.
Shule binafsi zipo mpaka za laki nane na ukute unalipiwa na michango ya ukoo. Hapo unatoa wapi uthibitisho kuwa umesomeshwa?
Kama wameamua kukopesha kwa nini wasikopeshe kwa kila aliefaulu kama anahitaji mkopo? Hiyo pesa inatokana na familia maskini tu au ni kodi ya watanzania wote?
Kwa nn vigezo isiwe ufaulu?
 
Hilo la kuwanyima mikopo wale waliyosoma shule za private halijakaa sawa...

Endapo ubaguzi utaendekezwa kwenye mikopo, basi hata kwenye ajira itafikia kwamba waliyosoma private wakafanye kazi private...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom