Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Huu mradi yaani umekua jinamizi kwa wakaazi wa Dar, japo MATAGA huwa yanasifia humu. Naomba sana tusije kurudia makosa ya Tanzania, tuwe makini sana na kutumia ubongo sio ujinga na ubabe usio na tija.
Mokosa yepi yaliyofanyika? Mbona hujayataja?
 
Huu mradi yaani umekua jinamizi kwa wakaazi wa Dar, japo MATAGA huwa yanasifia humu. Naomba sana tusije kurudia makosa ya Tanzania, tuwe makini sana na kutumia ubongo sio ujinga na ubabe usio na tija.

WHATEVER YOU SAY MKOPO WA WORLD BANK UPO PALE PALE, LAZIMA ULIPWE.!
 
Yani Afria sjui tukoje aisee, sijajua mpaka sasa jambo gani tunaweza lifanya Kwa usahihi.

Yani mradi wa Mwendokasi unakufa na wasimamizi wako kabisa halafu baadaye kwenye makongamano wanasimama kusema wazungu wanatuhujumu

Ifike wakati na vijana waaminiwe wapewe kusimamia miradi kama hii.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?

Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.

Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.

Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.

Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro



==========

UBUNGO: Kinachoendelea waziri mkuu anauliza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mabasi yaliyokwama ambapo mtu TRA anasema sheria inamruhusu kamishna kuya-donate au kuyaharibu na waziri mkuu amesema hawezi kupewa Shabiby kwasababu hayamfai kwenda Dodoma kwani ni kwaajili ya barabara za mwendokasi na sasa anauliziwa mwanasheria

Pia waziri mkuu anawaambia forodha waendelee kufanya minada ya mizigo iliyokaa kupita kiasi mara kwa mara ili kusafisha nafasi ya kuagiza mizigo mingine na kuwataka wabadilike kwani baadhi ya wateja wanalalamika process zinachukua muda mrefu

Kassim Majaliwa anasema pesa zilizotumika zimekopwa world bank na zinalipwa na mabasi yameletwa na mjasiriamali laiki ameshindwa ku-comply na sheria na sheria zimechukua mkondo wake tangu 2018 na kutaka kesho wakae waamue

Majaliwa amesema serikali inao uwezo wa kununua mabasi lakini tatizo ni usimamizi na hawawezi kumsimamia msimamizi ambae hawezi na leo amemuweka pembeni mkurugenzi wa fedha na mwingine anamuachia Rais kwani yuko kwenye mamlaka yake.

ZAIDI....

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Suzana Steven Chaula baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo wakati alipotembelea kituo Kikuu cha DART-Gerezani ambapo alionesha kutoridhishwa na utendaji wa viongozi hao akieleza kushangazwa katika kipindi cha miaka mitano hakuna basi hata moja lililonunuliwa na wakala wa mradi huo.

Katika ziara hiyo hiyo Waziri Mkuu ametembelea karakana ya UDA ya Kurasini, Dar es Salaam na kushuhudia baadhi ya mabasi ya wakala huo yakiwa mabovu na alipouliza yanakabiliwa na changamoto gani akajibiwa kuwa yanatatizo la mfumo wa gia (Gearbox) kitu ambacho amebaini kuwa ni uongo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea Kituo cha Forodha Bandari Kavu iliyopo Ubungo mkoani Dar es Salaam na kumuagiza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam, Njaule Mdendu kuhakikisha mizigo ya wateja katika bandari hiyo inatoka kwa wakati.

Waziri Mkuu amesema kuwa tangu mradi wa Mabasi yaendayo haraka DART ulipoanza mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85 huku wahusika wakikaa ofisini na kuacha wananchi wakiteseka.


Shamba la bibi hili, mtu akitenguliwa pahala analetwa hapa kuja kuchota za kujengea hekalu lake huko Mbweni, baaada ya mwaka anahamishwa tena anapewa ukuu wa moa analetwa mwengine naye achote tena.
 
Kazi kazi.

Mapigaji yanataka kurudi.

Safi sana waziri mkuu
Miaka 60 imepita, kila pahala ni mtindo huu huu. Eti anatokea mtu na heshima zake akihoji- HIVI WEMYEWE HATUWEZI". Halafu waumini wake wakiitikia mwimbo huo kwa shangwe sanaaaa.

Ndugu zanguni, watanzania wenzangu wakati umefika wa kuchukua maamuzi magumu. Tuwaunge mkono viongozi wetu walio liona hilo na kuchukua hatua mbadala kabisa. Umejaribiwa na kupewa nyenzo zote umeshindwa. Kwanini tusigeuze muelekeo na kuwapa wengine wenye uzoefu wa kuendesha shughuli kama hizo hata kama wanatoka mataifa mengine?
 
Kama mtoa huduma bado ni samson group mjue hatuendi popote. Hao watapeli hawawezi kuaminika kutoa huduma nzuri. Kwanza sifa ya mwekezaji hawana wanategemea waibie serikali kwaza ndio wawekeze.

Lengo lao kuu ni kupata mali kwa kuiba mali ya umma kujitajirisha. Uwekezaji ni kuleta mtaji na ujuzi sio ubabaishaji mtu huna kitu.
Ukifanya hivyo, eti watatokea akina Mwambukusi na vikundi vyake na kupinga. Eti kwa kigezo kuwa wenyewe tunaweza. Kazi kweli kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom