Uchaguzi 2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apasua ngome ya Mbowe Hai

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Waziri Mkuu Kasim Kajaliwa amebomoa Ngome ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge anaye maliza muda wake Freeman Mbowe kwa kusema hai ilikosa Mbunge kwa muda wa miaka kumi na tano.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la hai pamoja na kumwombea Kura Mgombea Urais wa CCM john Pombe Magufuli kura za ndio kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania kwa miaka mitano tena.

Majaliwa amewaambia wananchi wa hai waache ushabiki wa kuchagua viongozi wasio na uwezo Bali wachague mtu mwenye uwezo wa kutatua matatizo yao na kuwasikiliza wapiga kura wake na atakaye kaa jimboni.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hai imekosa maendeleo ya haraka kwa sababu mwakilishi wake akuwa na mipango ya kuleta maendeleo ya chap chap kama wabunge wengine.

Majaliwa amewaomba wananchi wa jimbo la hai kumchagua mgombea ubunge wa Ccm, Saasisha Elinikyo Mafuwe. ili aweze kuleta maendeleo hai kwani atapingana na serikali yake.

Amesema hai tumemtumia kijana msikivu Lengai Ole Sabaya kusimamia maendeleo kwa sababu Mbowe amekua akipinga kila kitu na kushindwa kuwa mwakilishi wa wananchi kwani mambo mengi wanapingana na serikali na kutoka nje ya bunge.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa hai ameomba kura kwa kusema kwamba hatasimamia miradi yote ya maendeleo katika jimbo la hai ndani Siku mia moja ikiwemo miradi ya Maji Afya Elimu na miundo mbinu ya bara bara.

Amewaomba wananchi kumpa kura na kumpima kwa muda wa miaka mitano waone utendaji wake wa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na madiwani wa halmashauri ya Hai.

Mgombea ubunge wa Siha Mollel amesema Mbowe hafai kuwa Mbunge tena kwa sababu amekuwa akitumia fedha za mfuko wa jimbo vibaya hivyo asichaguliwe na wananchi tena

Meya mstaafu wa jiji la Arusha kalisti Lazaro katika kampeni hizo amemwelezea mbowe kuwa ni kiongozi asiye jitambua hasa kupingana na serikali na kuwashawishi wabunge na madiwani wake kupinga maendeleo

Kalisti amesema alikua Chadema ameongoza baraza la madiwani kwa miaka mitano amekuwa akiambiwa apingane na serikali na hata muda mwingine avunje baraza iyo yote ni kuonyesha kupingana na serikali.

.
IMG_20200908_154048_7.jpg
IMG-20200906-WA0018.jpg
IMG_20200908_160011_4.jpg
IMG_20200908_171043_0.jpg
IMG_20200908_154027_5.jpg
 
Mkuu, Mbowe huko anaitwa ni Kaka, kwa taarifa yako huyu ni mwanafamilia ktk kila kaya na anakubalika ktk kila familia. Nakuhakikishia wale wahuni wa UVCCM waje tena na fujo zao tena ktk kipindi hiki cha kampeni chini uratibu wa mkora Sabaya ndiyo CCM watatambua ukweli wa mambo.
 
Ametia aibu Sana jana kule Moshi. Waziri mkuu mzima anahutubia watu 10b?!
 
Huyu naye ameanza kuchanganyikiwa. Aache kuangaikia majimbo ya wengine, akapambanie jimbo lake la sivyo atalikosa.

Anaposema Haiilikosa maendeleo kwa sababu ya mbunge, je mbunge anakusanyaga kodi? Hao wananchi wa hai wanapaswa wajue adui wao mkubwa aliye wanyima maendeleo ni CCM na serikali yake, huyo aliyejailiwa akiwa mmoja wapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom