Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aonya barua za Serikali kusambaa WhatsApp, Instagram

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.

Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.

“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema

Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.

Mwananchi
Aongee na wafanyakazi wake si kutuambia sisi maana akina kigogo wapo wengi serikalini
 
Umma sio watumishi. Na sijasema barua za siri

Kuna correspondences za ndani kwa ndani,kuna taarifa kwa uma na taarifa za siri mkuu
Sasa kama ni hivyo basi inakuaje zinasambaa kwenye magroup ya whatsapp?
Kwanini asiachie ngazi kwa kutoheshimika na kudharauliwa na watumishi hivyo?
Inakuaje anasimamia watu ambao hawana maadili halafu analia lia
Je sisi tumsaidieje?
 
Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
Alisema Yupo Ikulu Sasa Ameficha Siri Gani?Kwaiyo Siri nikusema Uongo Kwenye Mambo yanayogusa Taasisi nyeti Ya Urais?..Angechagua Kukaa Kimya Tu,Mbaya Zaidi anasema Uongo Msikitini Dah.
 
Acha kuwa zumbukuku ww,uongo hautakiwi kwa nafasi yake kwn kuumwa ni jambo la ajabu???wameumwa mitume itakuwa yule aliyejiita jiwe kumbe mrenda ?????
Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
 
hawa wameshalishwa ujinga na yule bi.Krembwe wendazke
Alisema Yupo Ikulu Sasa Ameficha Siri Gani?Kwaiyo Siri nikusema Uongo Kwenye Mambo yanayogusa Taasisi nyeti Ya Urais?..Angechagua Kukaa Kimya Tu,Mbaya Zaidi anasema Uongo Msikitini Dah.
 
"Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza." -- Haya ni mambo ya kupigwa vita kwenye katiba mpya.

Utendaji wa haki na usawa una nini cha kuficha?
 
Siri zimegawanyika mara 3.
1. Confidential
2. Secret
3. Top Secret

Zote hazitakiwi kusambaa mitandaoni
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom