Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 47,373
- 40,414
Wapigiane simu sasa kama ni siri
Majaliwa tangu atoe kauli yake ile "Rais yupo mzima na anachapa kazi ikulu"..nimemtoa thamani kabisa hafai tena kuwa kiongozi
Aongee na wafanyakazi wake si kutuambia sisi maana akina kigogo wapo wengi serikaliniWaziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.
Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.
“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema
Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.
Mwananchi
Sasa kama ni hivyo basi inakuaje zinasambaa kwenye magroup ya whatsapp?Umma sio watumishi. Na sijasema barua za siri
Kuna correspondences za ndani kwa ndani,kuna taarifa kwa uma na taarifa za siri mkuu
Alisema Yupo Ikulu Sasa Ameficha Siri Gani?Kwaiyo Siri nikusema Uongo Kwenye Mambo yanayogusa Taasisi nyeti Ya Urais?..Angechagua Kukaa Kimya Tu,Mbaya Zaidi anasema Uongo Msikitini Dah.Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
Alisema Yupo Ikulu Sasa Ameficha Siri Gani?Kwaiyo Siri nikusema Uongo Kwenye Mambo yanayogusa Taasisi nyeti Ya Urais?..Angechagua Kukaa Kimya Tu,Mbaya Zaidi anasema Uongo Msikitini Dah.
Kama wajitapa bar unanijua Mimi nani baada ya kusotea ajira wataweza vipi kuvumiliaVijana wataelewa basi🙄🙄
🤔kudhibiti utandawazi
Unapoteza muda wako, hao ni wanafunzi hawajawahi hata kuona masjala ya wazi Achana na masjala ya siriBarua za taarifa ni tofauti na barua za siri
Hajawahi kuwa sawa wala kumuelewa siku zote, jamaa yupo yupo tuHuyu bwana Majaliwa ni afadhali amfuate màgufool huko jehanum maana kama vile hayuko sawa hapa Duniani
Unataka awe nani, Uwe wewe?😂Afu huyu ndio mlikuwa mnasema anafaa kuwa prezdaa