Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,861
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.
Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.
“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema
Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.
Chanzo: Mwananchi