Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aonya barua za Serikali kusambaa WhatsApp, Instagram

Luckman1

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
2,681
2,000
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.

Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.

“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema

Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.

Mwananchi
Sasa zitafikaje ontime kwa Wadau?
Ndomana hata Serikali kuu inaweka insta, pia wanatuma WhatsApp groups kupitia kwa wasemaji wao.
Aache hizo mambo, barua za siri zinajulikana.
Zinakua na mhuri wa siri pia.
Hivyo, aache taarifa zifike kwa watu kwa wakati
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,766
2,000
Majaliwa tangu atoe kauli yake ile "Rais yupo mzima na anachapa kazi ikulu"..nimemtoa thamani kabisa hafai tena kuwa kiongozi
Mkuu Fukara achana na mawazo ya kifukara. Kifo ni ndani ya dakika moja tu. Waziri Mkuu aliongea siku chache kabla JPM hajapiga ndoo teke.
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
18,016
2,000
Kushare wasap au ig hakukwepeki maana nyingi hutolewa for public consumption
 
Mr kiuno

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
813
1,000
Sajili lain yako ya uwakala kwa MAJINA yako
Tgo pesa 120000/
Airtelmoney 60000/
Halopesa 25000/
M-pesa 145000/
M lipa 50000/
Malipo baada ya kazi
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,369
2,000
Sasa kama ni hivyo basi inakuaje zinasambaa kwenye magroup ya whatsapp?
Kwanini asiachie ngazi kwa kutoheshimika na kudharauliwa na watumishi hivyo?
Inakuaje anasimamia watu ambao hawana maadili halafu analia lia
Je sisi tumsaidieje?
Hahahaha hapo ndo patamu mkuu. Kila mtu analalamikà hadi mwenye madaraka analalamika
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Barua yoyote unayotuma kwa njia ya email hiyo haiwezi kuwa siri.
Labda kidigo fax.
Barua za siri akachukue mhusika mwenyewe.
Tatizo liko hukohuko juu ndio maana tunaona teuzi zinatangazwa usiku
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
6,017
2,000
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.

Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.

“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema

Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.

Chanzo: Mwananchi
Anaataka zisisambae anataka tuzisomee kwyenye gazette la serikali au?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,130
2,000
Mlikuwa hamuelewi magufuli alivyowaeleza mawasiliano ndani ya serikali yafanyike kwa kutumia makaratasi, mnajifanya wajuaji kuanzisha makundi yenu ya wasap, taasisi za serikali unakuta taarifa zinatolewa kwenye magroup ya wasap......kama hujajiunga taarifa nyingi za ofisi zinakuwa zinakupita yaani hata mbao za matangazo hazina umuhimu tena, hovyo kabisa.....
 
NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,708
2,000
Umma sio watumishi. Na sijasema barua za siri

Kuna correspondences za ndani kwa ndani,kuna taarifa kwa uma na taarifa za siri mkuu

Mawasiliano hupangwa na kuratibiwa. Kama ni siri mawasiliano hayo yataainishwa hivo. Kama sio siri, haitatajwa ni siri. Ukimwandikia mtu barua, huwezi ukaifanya siri. Siri haiwezi kuwa katika taarifa - inakuwa katika kufahamisha maamuzi!!
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,369
2,000
Mawasiliano hupangwa na kuratibiwa. Kama ni siri mawasiliano hayo yataainishwa hivo. Kama sio siri, haitatajwa ni siri. Ukimwandikia mtu barua, huwezi ukaifanya siri. Siri haiwezi kuwa katika taarifa - inakuwa katika kufahamisha maamuzi!!
Wewe barua ukiandika kwa demu wako hua unaainisha kwamba ni siri??? Na hio barua ukiikuta mtandaoni utaona ni sawa??? Sema kiswahili kina misemo hafifu. Kuna vitu Private ni kwa matumizi ya wahusika tu,sio public knowledge kipi kigumu hapo
 
cyrustheemperor

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
262
500
Anaesema WAZIRI mkuu anaongea Jambo la maana sana anyoshe mkono juu.Sijui watanzania tunachaguaje viongozi katika Zama hizi za utandawazi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom