Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aonya barua za Serikali kusambaa WhatsApp, Instagram

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,840
2,000
1625125829746.png

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.

Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.

“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema

Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.

Chanzo: Mwananchi
 

Fukara

JF-Expert Member
Dec 28, 2013
1,601
2,000
Majaliwa tangu atoe kauli yake ile "Rais yupo mzima na anachapa kazi ikulu"..nimemtoa thamani kabisa hafai tena kuwa kiongozi
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,369
2,000
Hizo barua zinahusu nini!?
Kama zinawataarifu watumishi basi hizo sio za siri tena
Hata kama zitakua ni za ndani kwa ndani
Umma sio watumishi. Na sijasema barua za siri

Kuna correspondences za ndani kwa ndani,kuna taarifa kwa uma na taarifa za siri mkuu
 

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,035
2,000
Majaliwa tangu atoe kauli yake ile "Rais yupo mzima na anachapa kazi ikulu"..nimemtoa thamani kabisa hafai tena kuwa kiongozi
Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom