Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aombwa kurudi kuzindua barabara mwishoni mwa mwezi wa 11

mchumihalisi

Member
Oct 8, 2015
27
75
Mimi ni mmoja kati ya watu waliokua wanaifatilia Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa Mikoa ya kusini mwa Tanzania, Pamoja na kwamba Ziara nyingi za PM akiibuka sehemu hapakosi jambo au kumuacha mtu salama Lakini nilikua najiuliza WHY PM hakumpa nafasi Naibu Waziri aelezee suala la kukosekana kwa Taa kwenye ile Barabara mpya ya Lami ya Liwale?

Nikahisi labda kuna kitu anataka kutuficha lakini Baada ya kuona Clip ya Naibu Waziri akijielezea kwenye Kikao cha Watendaji nimeona dhahiri Waziri Mkuu alikua sahihi kutozindua ile Barabara, ambayo huenda mbele ya Safari tungekuja kuhoji kakubali vipi kuzindua kitu ambacho hakijakamilika, Ingekua kuweka Jiwe la Msingi isingekua neno.

Nimeona Kistaarabu Naibu Waziri Ujenzi Mh. Kasekenya amekiri kwanza kuwa ni tatizo na kusema kuwa wameanza kufanyia Kazi na tayari wamewasiliana na TANROADS ili kufika mwisho wa mwezi November (11) TAA ziwe zimewaka Maeneo yote ya Mji wa Liwale.

Kongole Waziri Mkuu Majaliwa tunaamini bado ni mshauri mzuri wa Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu na mnaendelea kuhakikisha pesa za Wanyonge kwenye Serikali hii ya awamu ya Sita haziibiwi.

Kwa ushauri tu Wakandarasi na Baadhi ya Watendaji wa Serikali acheni Ujanja ujanja. Serikali iko Macho hii, Mama alisema pamoja na kwamba mnaona macho yamelegea LAKINI yanaona.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom