Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Wamachinga kitaifa na uzinduzi Wamachinga Saccos

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
KONGAMANO LA WAMACHINGA KITAIFA NA UZINDUZI WA MACHINGA SACCOS

Shirikisho la Wamachinga (SHIUMA) Kwa kushirikiana na Machinga Mkoa wa Dar es salaam wanakukaribisha kushiriki (kufuatilia) Uzinduzi wa Machinga SACCOS utakaofanyika katika kongamano la Kitaifa la Wamachinga.

Saccos ya Wamachinga imelenga kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa Wamachinga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kukuza Biashara zao.

Kongamano litahusisha Wamachinga kutoka nchi nzima kupitia wawakilishi wao kutoka kila Mkoa, na litafanyika katika Ukumbi wa PTA - SABASABA, Dar es salaam, Februari 19, 2022 kuanzia Saa Mbili asubuhi (8:00am)

Mgeni Rasmi katika tukio hili anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa.

Kongamano hili limedhaminiwa na Benki ya CRDB.

IMG-20220213-WA0510.jpg
 
Atapigwa chini soon.... Chifu Hangaya na wamachinga wapi na wapi? Chifu Hangaya alishasema wamachinga ni uchafu kwa wawekezaji. Sisi tunaona watu wa Chifu wakiendelea kufukuza wote wanaojihusisha na micro businesses (wamachinga).

Masoko yao yanachomwa na wasiojulikana. Mtetezi wao ameshageuka mifupa (skeleton).

PM aache kuwahadaa wamachinga.
 
Ajibu kwanza kwanini alituhadaa kuwa kiongozi yupo ofisini kumbe yu mahtuti kitandani
Umenikumbusha mkuu. Aliutangazia umma kuwa kiongozi ni mzima na anachapa kazi kumbe tayari yuko jehanamu.

Inabidi siku ya hilo kongamano atoe maelezo ya kina
 
Umenikumbusha mkuu. Aliutangazia umma kuwa kiongozi ni mzima na anachapa kazi kumbe tayari yuko jehanamu.

Inabidi siku ya hilo kongamano atoe maelezo ya kina
Huyu alipelekwa mkoani huko kufanya ziara akidanganywa na akina Bashiru.

Lakini kauli yake ipo siku itamponza.
 
Umenikumbusha mkuu. Aliutangazia umma kuwa kiongozi ni mzima na anachapa kazi kumbe tayari yuko jehanamu.

Inabidi siku ya hilo kongamano atoe maelezo ya kina
Hii dhambi hawezi kuikwepa abadan😉
 
Huyu alipelekwa mkoani huko kufanya ziara akidanganywa na akina Bashiru.

Lakini kauli yake ipo siku itamponza.
Halafu kaitwa mheshimiwa kumbe mdanganyifu, mmmh!!! Nchi hii tumerigwa,
 
Mwenzake aliambiwa atubu na yeye atubu kwa kuudanganya umma wa Tanzani

Back
Top Bottom