Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amwakilisha Rais Magufuli kwenye mkutano wa kupambana na rushwa, London

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amwakilisha Rais Magufuli Kwenye mkutano wa Kupambana na Rushwa, London.

IMGS4852.JPG.jpeg


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa kuingia kwenye ukumbi wa Lancaster House, London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Mei 12, 2016. Waziri Mkuu Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.

BM7T8171.jpg


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kulia) akishiriki katika Mazungumzo Rasmi ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwenye ukumbi Lancster House, London, nchini Uingereza Mei 12, 2016. Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Safi sana ngoja na wengine wapate uzoefu kwa manufaa ya taifa letu. Maana tulikuwa tumewazoea walewale kila siku.
 
Magufuli hana tabia ya kupenda safari. Sidhani kama waziri mkuu atakuwa ameandamana na rundo kubwa la watu. Miaka kadhaa iliyopita mkuu wa nchi alibeba watu zaidi ya 50 kwenye msafara mmoja wa Marekani!. Halafu ni kiongozi wa nchi ambayo wanafunzi wa shule ya msingi wanapata matatizo ya migongo kwa sababu ya kukaa sakafuni.
Hili la kubana matumizi ni jema sana.
 
Awe anamtumia huyu,kidogo anaweza kujieleza akaeleweka!

Dah nimecheka kuna mengine yanakaukweli laikin dah......JPM asingechelewa hapo kusema halmashauri ya Inkasi inawafanyakazi hewa 257.4 na fisadi mmoja....
 
Kama washiriki hawataweza kutoka na azimio la pamoja kuyataka/kuyabana mabenki kuwa na uwazi kwa swala la wakuu wa nchi maskini kutoreshea fedha kwenye mabenki ya nje, watakuwa hawana nia ya dhati kupiga vita ufisadi mkubwa!
 
Naomba kwanza ni declare interest.

Mimi ni Ukawa damu, lakini kwa hili nasema safi sana kwa Magufuli kutotokwenda kwenye hicho kikao.

Hao wazungu (waingereza) wao ndio wala Rushwa wakubwa hapa duniani na hata hapa Tanzania tumeona kupitia mikataba ya madani.

Halafu Leo hii ndio wanatupa lecture za rushwa na kutuita "fantastically corrupt" countries
 
Uingereza nayo imejichokea huo ukuta utadhani Tandale.View attachment 346955


Hawa jamaa huwa Ni wataalam wa kupiga picha tuu, huwa wanabalance sana, hawapendi Kutoa sehemu zilizochoka, au kuonekana taka taka, kwa mfano ukiona kwenye tv mazingira, Na ukenda kuyafuma utashangaa. kamera Hapa itakua wameteleza tuu.
 
Hawa jamaa huwa Ni wataalam wa kupiga picha tuu, huwa wanabalance sana, hawapendi Kutoa sehemu zilizochoka, au kuonekana taka taka, kwa mfano ukiona kwenye tv mazingira, Na ukenda kuyafuma utashangaa. kamera Hapa itakua wameteleza tuu.
Kwanini na kwenu msifanye hivyo? (mwafrika haishiwi sababu!!!!)
 
Back
Top Bottom