Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Tukio la mauaji ya mfanya biashara wa madini yaliyofanywa na polisi limeonyesha dhahiri kuwa kuna upungufu mkubwa katika usimamizi wa haki hapa nchini. Baada ya taarifa kuonyesha kwamba polisi walihusika na mauaji hayo, ingetegemewa.

kwamba vyombo vinavyosimamia sheria vingetoa tamko mara moja, hususan polisi kuanza uchunguzi wa tukio hilo wakati
polisi hao hao ndio waliokuwa wanahusika.

Ingetegemewa kwamba mathlani waziri wa katiba na sheria au waziri wa mambo ya ndani au hata waziri mkuu toe tamko la kutaka chombo kingine nje ya jesho la polisi ndo lifanye uchunguzi. Lakini tumeona.

Hao wote niliowataja hapo juu walikuwa wamelala hadi Rais alipomwagiza Waziri Mkuu aunde kamati ya kufanya uchunguzi
huo. Ni muhimu mfumo wa kusimamia na kutoa haki ufanye kazi bila kusubiri hadi Rais aseme ndo haki itendeke. Vinginevyo
Rais akipotezea haki nayo inapotea.
 
Back
Top Bottom