Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa EWURA

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,447
2,000
Wanabodi tumbua imeendelea tena usiku huu nasoma hapa kwa uhakika kabisa Bwana Ngamlagosi ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA amesimamishwa kazi na Waziri Mkuu.

Sababu za kusimamishwa hazijatajwa. Pole bwana Felix haya madaraka ya umma magumu sana.

IMG-20170611-WA0011.jpg
 

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,305
2,000
IMG_20170611_011215.jpg


Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ndugu Felix Ngamlagosi Kuanzia leo Tarehe 11/06/2017.

TAARIFA ILIYOTOLEWA NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI.​
IMG_20170611_011305_300.JPG
 

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,057
2,000
Itakua IPTL au kupandisha bei mafuta, haya mambo ya mikataba hayatawaacha wakurugenzi wa mashirika ya umma salama kwa sababu tu ya siasa lakini pia hayatatuacha nchi salama.

Huyu bwana hakujifunza kutoka kwa mwenzake aliepandisha bei ya umeme kwa kufuata taratibu zote kisha akatenguliwa ukurugenzi, yeye kapandisha bei mafuta kwa kufuata utaratibu mwisho ndio hayo yanayomkuta.

Nimeona tweet ya msemaji wa serikali.
Screenshot_20170611-011759.png
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Alitakiwa afanye nini kama sababu ni kuipa leseni IPTL mkataba watengeneze wengine lawama arudishiwe mtoa leseni. Seriously on what ground anaweza wanyima IPTL leseni wakati wanamkataba wa kuzalisha umeme.

Spare a thought to the chap ndio si hasa zetu hizo mbuzi wa kafara lazima atafutwe halafu mwisho wa siku IPTL watapewa tu leseni yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom