Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Wilaya ya Same

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mhandisi wa maji wa Wilaya ya Same, Mussa Msangi kutokana na kushindwa kusimamia utekelezaji wa mradi wa maji Hedaru.

Pia, amezivunja jumuiya tatu za maji Hedaru na kuagiza viongozi wa wake kukamatwa na kuhojiwa kuhusu mapato yatokanayo na mradi huo.

"Kamanda wa polisi nitafutie viongozi hawa wa maji walete hapa waniambie kwa nini wananidanganya, utaondoka nao hawa," amesema Majaliwa leo Ijumaa Julai 19, 2019 baada ya kufika eneo la uzinduzi na kukuta maji hayatoki.

Kufuatia hali hiyo Majaliwa pia alimtaka naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso kubaki Hedaru kwa siku tatu kuhakikisha anashughulikia changamoto iliyojitokeza katika mradi huo.

Akijitetea, Msangi amesema maji yapo lakini tatizo mradi huo umetumia sola na unapokuwa na mawingu maji yanasumbua, sababu ambayo Majaliwa aliipinga.
 
Safi Sana, aende na Rombo shida ya maji ipo tangia uhuru na hao wahandisi wanatafuna tu pesa za miradi ya Maji
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mhandisi wa maji wa Wilaya ya Same, Mussa Msangi kutokana na kushindwa kusimamia utekelezaji wa mradi wa maji Hedaru.

Pia, amezivunja jumuiya tatu za maji Hedaru na kuagiza viongozi wa wake kukamatwa na kuhojiwa kuhusu mapato yatokanayo na mradi huo.

"Kamanda wa polisi nitafutie viongozi hawa wa maji walete hapa waniambie kwa nini wananidanganya, utaondoka nao hawa," amesema Majaliwa leo Ijumaa Julai 19, 2019 baada ya kufika eneo la uzinduzi na kukuta maji hayatoki.

Kufuatia hali hiyo Majaliwa pia alimtaka naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso kubaki Hedaru kwa siku tatu kuhakikisha anashughulikia changamoto iliyojitokeza katika mradi huo.

Akijitetea, Msangi amesema maji yapo lakini tatizo mradi huo umetumia sola na unapokuwa na mawingu maji yanasumbua, sababu ambayo Majaliwa aliipinga.
Hizi hukumu za majukwaani ni tabu. Zina madhara makubwa kwa watu binafsi, serikali, jumuiya na mfumo wetu wa kisheria. Juzi tumeona polisi waliokwisha fukuzwa bahada ya hukumu za majukwaani wakifutiwa mashitaka na kurudishwa kazini. Pamoja kwamba inashangiliwa na sifa kemukemu, lakini ina athari katika mfumo wetu wa sheria. Ina ugumu gani ikiwa kuna kosa kuacha mchakato wa kisheria ufanyike na matokeo yake ndiyo yatolewe! Badala yake tunahukumu kisha mchakato unafuata - na matokeo yake hata yakionekana kuwa mtuhumiwa hana hata hayamsafishi muhanga mbele ya jamii. Si haki hata kidogo.
 
Back
Top Bottom