Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Afisa Manunuzi Wilaya ya Karagwe kwa kutoridhishwa na ujenzi wa Hospitali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Manunuzi wa Wilaya ya Karagwe Bw. Yesse Kaganda baada ya kutoridhishwa na viwango vya ubora wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe ambayo imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5.

“Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kila wakati anasisitiza usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa ili zitumike kwa ukamilifu na kujenga miradi yenye ubora, vigae hivi havijaanza kutumika tayari vimechakaa, Afisa Manunuzi huyu akae pembeni kwanza na vigae vipya viwekwe kwa gharama zake.”

Waziri Mkuu amesema Rais Mheshimiwa Samia ametoa pesa za kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo na kuhakikisha Serikali inasogeza huduma zote muhimu za kijamii lakini watendaji wachache wamekuwa wakishindwa kufuata maadili ya kazi zao na kujenga miradi isiyokuwa na ubora.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 19, 2021) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanasimamia vyema matumizi ya fedha zilizotolewana Rais Mheshimiwa Samia katika kutekeleza miradi ya maendeleo na huduma za jamii ili kuleta tija na mabadiliko kwa wananchi.

“Malengo ya Rais wetu sasa yanaenda kutimia kwani anataka kila mwananchi apate huduma za afya hukohuko aliko, kuanzia ngazi ya kijiji tunajenga zahanati na baada ya kuwa zahanati za kutosha tunajenga kituo cha afya ambacho kina huduma zote muhimu, kama upimaji wa magonjwa yote, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto pamoja na wodi za wanaume na wanawake”. Alisema

Waziri Mkuu amewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Karagwe kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo utakamilika kwa wakati na kwa viwango kwani tayari fedha za kununua vifaa tiba vyote na mitambo ya mionzi zimetengwa.

Amesema wananchi pia wana wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa maoni kwani miradi hiyo inatekelezwa kwa kodi za wananchi. “Ninawaomba wananchi muendelee kuwa na imani na Serikali yenu pamoja na viongozi wake,"​

IMG_20210920_070622_036.jpg
 
Lakini all in all, Afisa manunuzi anaonewa. Sikuzote Afisa manunuzi anafuata specifications za Mhandisi. Kama ameleta kitu ambacho Mhandisi hakuspecify, huwa lazima kinakataliwa!
Apresent documents za requests kutoka kwa Mhandisi. Kama alicholeta ndicho kinareflect kwenye documents, hana kosa.
 
Uko sahihi sana mkuu, ila tatizo ni kuwa watu wanaangalia ni nani alienunua (Alie-place Orde), na sio ni nani alie-request. Nina uhakika kwa utaratibu wa serikali, lazima hapo wilayani kuna "Procurement committee", ambayo ilihusika. Kuna pia Engineer alietoa specifications; kuna pia "Receiceving committee" ambo waiopokea na ku-confirm kuwa hivyo vigae vinaendana na "request" na "Purchase Order". Ila sasa "likipinda" kila mtu anatafuta jinsi ya kujitoa na kumsukumia mwenzake.
 
Ipo B0q, wapo walio idhinisha manunuzi,mapokezi na kusimamia ujenzi ili mzabuni au mkandarasi alipwe... Huyo kaonewa au katorewa kafara...

Hizo ni siasa hamna kitu hapo...
 
Ndio hicho nilichoeleza hapo. Afisa manunuzi wa serikali hana mamlaka ya kuamua kununua nini na wapi peke yake - taratibu hazimruhusu, kuna watu wanaotayarisha hizo specifications na pia kuna "Procurement Commitees". Sasa kwa nini awekwe pembeni yeye peke yake, na hao wengine wawe salama?
 
Kwani hukuna mkandarasi kwenye huo ujenzi ? au ndio mambo ya kutumia mafundi mchundo.
 
Uko sahihi sana mkuu, ila tatizo ni kuwa watu wanaangalia ni nani alienunua (Alie-place Orde), na sio ni nani alie-request. Nina uhakika kwa utaratibu wa serikali, lazima hapo wilayani kuna "Procurement committee", ambayo ilihusika. Kuna pia Engineer alietoa specifications; kuna pia "Receiceving committee" ambo waiopokea na ku-confirm kuwa hivyo vigae vinaendana na "request" na "Purchase Order". Ila sasa "likipinda" kila mtu anatafuta jinsi ya kujitoa na kumsukumia mwenzake.
Aliyesaini Purchase Order ndiye aliyenunua. Maana naye lazima ajiridhishe na supporting documents!
 
Uko sahihi sana mkuu, ila tatizo ni kuwa watu wanaangalia ni nani alienunua (Alie-place Orde), na sio ni nani alie-request. Nina uhakika kwa utaratibu wa serikali, lazima hapo wilayani kuna "Procurement committee", ambayo ilihusika. Kuna pia Engineer alietoa specifications; kuna pia "Receiceving committee" ambo waiopokea na ku-confirm kuwa hivyo vigae vinaendana na "request" na "Purchase Order". Ila sasa "likipinda" kila mtu anatafuta jinsi ya kujitoa na kumsukumia mwenzake.
Hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu (ya kumsimamisha kazi A/Ugavi) ni sahihi kwani ndiye aliyenunua hizo 'tiles' mbovu na kama aliagizwa basi ni yeye atakayetoa taarifa/maelezo hayo kwa dola!
 
Mambo ya force account hayo tumtegemee mengi tungeweka contactor ...yasingetokea haya .. ni kuoneana tu.....menginyatakuja. Kuna hostel na mengineyo... Tusubiri

Kenya daraja limevunjika. On ongoingg contruction.... contractor tupo ndani bongo tunafukuza Procument....maajabu
 
Hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu (ya kumsimamisha kazi A/Ugavi) ni sahihi kwani ndiye aliyenunua hizo 'tiles' mbovu na kama aliagizwa basi ni yeye atakayetoa taarifa/maelezo hayo kwa dola!
Tenda ya ujenzi ilitangazwa au ilikuwa force account
 
Swali hilo nalo ni vyema ukamuuliza Afisa Manunuzi ndio maana amesimamishwa kazi awajibu wadau kama wewe na wengine!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom