Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aikaribisha Urusi kuwekeza kwenye reli

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways, Alexander Misharin na kumweleza kuwa Tanzania inahitaji kuimarisha usafi ri wa ndani wa reli hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga.

Amesema kampuni hiyo yenye uwezo mkubwa wa kujenga reli mpya, kukarabati, kutengeneza injini za treni na mabehewa na ukarabati wake inahitajika nchini ili kufanikisha mpango wa serikali wa kuimarisha reli za zamani za Tazara, ya Kati na kufungua ya Kaskazini inayounganisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Waziri Mkuu alizungumza na mkurugenzi huo juzi mjini Sochi nchini Urusi, ambako alitumia fursa hiyo kuikaribisha Russian Railways kuwekeza nchini hususani katika sekta ya ujenzi, ufundi na mafunzo ikishirikiana na kampuni za Watanzania. Waziri Mkuu yuko nchini Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi, uliotarajiwa kuanza jana jijini Sochi, akimwakilisha Rais John Magufuli.

“Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajenga reli ya kiwango cha kimataifa ya SGR pamoja na kufufua reli ya Kaskazini, inaikaribisha Kampuni ya Russian Railways kwa mikono miwili ije ifanye mazungumzo rasmi na Wizara husika. Pia Serikali inao mkakati wa kujenga reli mpya katika ukanda wa Kusini kutoka Mtwara hadi Ruvuma ili kuiunganisha bandari ya Mtwara na mikoa ya Kusini pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia,” alisema.

Alisema Tanzania kwa sasa inahitaji kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga hivyo endapo mazungumzo kati ya wizara husika na kampuni hiyo yataonekana kuwa na tija na yana maslahi kwa Watanzania, kampuni hiyo itapewa fursa ya kuwekeza nchini.
 
Kazi nzuri awamu ya tano

Kuna watu wanatukana serkali ila wanatumia barabara zilizojengwa na awamu ya tano
Unaweza kuona wasivyo na aibu
 
Nakumbuka Mwakyembe aliwahi kumkaribisha Diaspora mmoja kuwekeza kwenye railway Dar es Salaam, siku hiyo usiku nilikuwa nimekaa sehemu mpaka bia yangu ikaniparia kwa kicheko.
 
Waje kuwekeza kwenye ile #dirty# dangerous materials ili tupate Umeme wa kutosha. Pia tuki Zi enrich zaidi hizo material tutapata leverage ya ku dictate terms in corporate world.
 
Toka mwaka juzi naskia reli ya dar tanga had arusha imeanza kupg kazi na majaribio nikaskia na kuona kwenye tv yanafanyika kumbe ilikua haijakarabtiw tu. Tuachen siasa tufanye kazi. Kazi nzuri inaonekana na inajenga iman kwa wananchi.
 
Ndiyo maana tulisema toka mwanzo kuwa kumchukia mzungu na kumwita beberu kwa vile tu kakuzidi kila eneo na anakukemea unapovunja haki za binadamu, ni upumbavu.

Tanzania ili ipate maendeleo inahitaji sana uwekezaji mkubwa kutoka kwa hawa wazungu. South Korea wamefanikiwa kutokana na uwekezaji wa wazungu. Wachina wamefanikiwa kutokana na uwekezaji wa wazungu (bahati mbaya watu wengi kutokana na ujinga, wanafikiri wachina wamefanikiwa wenyewe kwa kujitenga na wazungu). Hali ni hiyo hiyo kwa mataifa kama Singapore, Malaysia, Saudia, Kuwait, UAE, n.k.

Hata yale mambo madogo kabisa ambayo hata mtu mwenye akili ya kawaida anayajua, wakuu wa serikali walifishwa na nini hata kuanza kujitutumua kwa mambo ambayo hawana uwezo nayo kabisa? Eti Tanzania inaweza kuisaidia hata Marekani. Ni sawa na kusema kuwa Liquid anaweza kumfadhili Bakhresa. Wanaokusikia lazima watatoka na mengi juu ya yako!
 
Back
Top Bottom