Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,214
728


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iandae semina kwa wabunge wote ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Februari 9, 2022) wakati alipochangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2021, Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema kuwa anaamini wapo wabunge wanaofahamu na wasiofahamau kuhusu yanaoendelea katika hifadhi hiyo “wakati tukiwa tunazungumza na wananchi, naiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya semina ya siku moja kwa wabunge wote ili wizara iwaambie kuna nini kule Ngorongoro, nini kilikuwepo awali na hali gani ipo sasa ili tuwe na uelewa wa pamoja”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali kukutana na wakazi wanaoshi katika eneo la hifadhi Ngorongoro na utekelezaji wake umeanza kwa kukutana na viongozi wa mkoa wa Arusha na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Hatua iliyobaki ni kwenda Ngorongoro, nitafanya mikutano eneo la Ngorongoro, nitafanya mikutano na wakazi wa eneo la Loliondo, baada ya kufanya haya yote itatusaidia kuendesha zoezi hili kwa amani kabisa kadiri itakavyokuwa imeamriwa”

Akizungumza wakati akichangia hoja ya kamati hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Wizara italeta mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya Ngorongoro kulingana na mapendekezo ya kamati na maoni ya wabunge.

“Sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1975 ni ya muda mrefu, mliyoongea Waheshimiwa wabunge yameonesha kuna mapengo kwenye sheria ile, msingi wa Sheria ile ni nguzo tatu za Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii, inaonekana nguzo hizi zimeshindikana kushikiliwa kwa pamoja”

Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia inajali haki za binadamu “hatutafanya chochote ambacho kiko kinyume na haki za binadamu, na kwa kuwa tunaheshimu haki za binadamu hatutaingilia uhuru wa vyombo vya habari”.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,348
22,252
CCM katika ubora wao;

Mwaka 2022;- "Wakazi wa Ngorongoro wapelekewe vifaru vya jeshi kuwatoa na mabomu ya machozi waondolewe. Kama vilipelekwa mtwara kwenye kuwaondoa wananchi kwenye gesi na korosho, huku kwanini visipelekwe kuwaondoa pia?".

Miaka mitatu baadae. . . .

Mwaka 2025;- "Wakazi wa Ngorongoro tupeni kura zenu, si mnaona maendeleo haya mliyonayo? Watalii ni wengi! Ma hoteli ya kisasa ni mengi! Ajira ni nyingi! CCM ndio inajali shida zenu. Yote haya maendeleo mliokuanayo ni katika kutekeleza ilani ya CCM"

Mungu ni mwema.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
20,758
16,244
“Sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1975 ni ya muda mrefu, mliyoongea Waheshimiwa wabunge yameonesha kuna mapengo kwenye sheria ile, msingi wa Sheria ile ni nguzo tatu za Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii, inaonekana nguzo hizi zimeshindikana kushikiliwa kwa pamoja”
Kwa mujibu wa Kitenge, ni utalii na uhifadhi ndivyo vina usumaku mkali wz kushikana pamoja!!!
Hiiiii! Aaii!
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,151
19,360
Sema anafichia aibu bunge la mazuzu,Kuna wabunge wameropoka kwamba wamasai wapelekewe vifaru,mwingine kasema wapelekewe washawasha na kuondolewa kwanguvu bila kujua kwamba wale wamasai wanaishi mle kihalali kwa sheria.

Ili kuwatoa mle lazima sheria ibadilishwe
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
5,122
5,628
Mnawafukuza wamasaai toka Ngorongoro na loliondo ambayo ni maeneo yao ya asili waende wapi? mmeisha waandalia sehem ya kwenda? hayoo mahifadhi na mambuga yenu yamewakuta wamaasai apo sasa sijui mnatakaje, basi waueni wamasaai wote mioyo yenu ilizikee sasa!
 

Simchezo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
421
320
Napendekeza wamasai wanaoishi hifadhini waondolewe, kuna competition kubwa ya chakula na maji kati ya wanyama pori na mifugo ya wamasai, idadi ya wakazi inaongezeka Kwa Kasi wakati eneo la hifadhi haliongezeki.

Tanzania ni kubwa wapelekwe sehemu nyingine na kupatiwa mahitaji yote muhimu kama malisho, maji ya uhakika, huduma ya afya, shule.....Ngorongoro sio ya wamasai peke Yao ni ya Watz wote...
 

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
968
1,070
Ndio Hifadhi wanaishi watu na wanyama
Sijakuelewa. Nilichouliza ni kwamba Serikali inataka kuwaaondoa watu kwenye hifadhi ya Ngorongoro ili wanyama waongezeke. Swali langu ni kwamba jee, ni Ngorongoro tu kunakokuwepo na mgongano wa watu na wanyama? Au kuna kitu kingine nyuma ya pazia kunakofanya hicho kiwe kisingizio?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
26,481
45,600
Sijakuelewa. Nilichouliza ni kwamba Serikali inataka kuwaaondoa watu kwenye hifadhi ya Ngorongoro ili wanyama waongezeke. Swali langu ni kwamba jee, ni Ngorongoro tu kunakokuwepo na mgongano wa watu na wanyama? Au kuna kitu kingine nyuma ya pazia kunakofanya hicho kiwe kisingizio?

Suala la Ngorongoro lina pande mbili.

1. Wanaoamini wanyama, binadamu, na mifugo, wanaweza kuishi pamoja.

2. Wanaoamini wanyama, binadamu na mifugo hawawezi kuishi pamoja.

Jamii ya Wamaasai walioko Ngorongoro walihamishwa toka maeneo ya mbuga ya Serengeti wakati wakoloni walipoamua Serengeti iwe hifadhi ya taifa.

Wamaasai wa Ngorongoro wamekuwa wakiishi na wanyama na kulisha mifugo yao bila matatizo kwa muda mrefu sasa.

Jamii hiyo ina uzoefu mkubwa wa kujua majira mbalimbali ya ukuaji na upatikanaji wa malisho na movement za wanyama kulingana na misimu ktk mwaka.

Kwa mfano majira ambayo nyumbu wengi huzaliana Wamaasai wanajua wapi pa kwenda kulisha mifugo.

Pia msimu wa nyumbu kuhama kwa makundi makubwa Wamaasai hujua jinsi gani na eneo gani wanaweza kuchunga mifugo.

Zaidi Wamaasai wanajua jinsi ya kutunza maeneo ya malisho. Kuna msimu wa kuchoma majani ili kuzuia magugu mabaya yasiote na kutoa nafasi kwa malisho mazuri kumea.

Zoezi la kuchoma moto maeneo ya Serengeti na ktk hifadhi hufanywa hata na serikali / TANAPA.

Kwa kifupi Wamaasai sio maadui wa wanyama au uhifadhi hapa Tanzania. Kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na utaratibu SHIRIKISHI huko Ngorongoro ili kila upande ufaidike.
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
5,122
5,628
Napendekeza wamasai wanaoishi hifadhini waondolewe, kuna competition kubwa ya chakula na maji kati ya wanyama pori na mifugo ya wamasai, idadi ya wakazi inaongezeka Kwa Kasi wakati eneo la hifadhi haliongezeki.

Tanzania ni kubwa wapelekwe sehemu nyingine na kupatiwa mahitaji yote muhimu kama malisho, maji ya uhakika, huduma ya afya, shule.....Ngorongoro sio ya wamasai peke Yao ni ya Watz wote…
Kwanini msi waondoe hao wanyamapori na kuwaachia wamasaai hayo maeneo yao ya asili ya loliondo na ngorongoro??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

7 Reactions
Reply
Top Bottom