Waziri Mkuu John Magufuli, mbona nchi ingenyooka hii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu John Magufuli, mbona nchi ingenyooka hii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Aug 25, 2011.

1. F

Fareed JF-Expert Member

#1
Aug 25, 2011
Joined: Apr 13, 2010
Messages: 328
Likes Received: 12
Trophy Points: 0
Kuna tetesi zimeanza kuwa Rais Kikwete huenda akavunja baraza lake la mawaziri baada ya kikao cha Bunge kinachoisha wiki hii. Kuvunja huku kwa cabinet itakuwa ni utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba kwa serikali kama ilivyokuwa kwa chama tawala. Ni ukweli usiopingika kuwa serikali imepwaya sana na kila mwananchi anaonesha kukata tamaa.

Rais, Waziri Mkuu na baraza la mawaziri wote wanaonekana ni legelege. Hivyo basi kuna haja ya kuvunja cabinet na kuunda jipya, mbinu ambayo hutumiwa na viongozi wengi kujaribu kuleta matumaini mapya pale ambapo serikali zao zinapokuwa zimepoteza imani ya wananchi kama ilivyo kwa serikali ya JK.

Tetesi hizi zimenifanya niote jinsi ambavyo nchi yetu ingenyooka kama JK angekuwa na ujasiri wa kumteua John Pombe Magufuli kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Magufuli amekuwa na rekodi isiyo na mfano wa kuwa mchapa kazi mahiri tangu serikali ya Mkapa. Si muoga wa kufanya maamuzi, ni mtu vibrant na wananchi wengi wanamkubnali. He is a no-nonsense leader na angeleta uhai mpya serikalini.

Kwa bahati mbaya najua kuwa ndoto zangu za kumuona mtu mwenye calibre ya Magufuli anakuwa PM haziwezi kutimia kwa sababu zifuatazo:

1. Rais Jakaya Kikwete (kama Marais wengi wa Afrika) hataki mtu amzidi umaarufu (outshine). Ndiyo maana alimchagua mtu kama Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu ambaye amepwaya sana kwenye nafasi hiyo mpaka wengine wanamkumbuka Edward Lowassa licha ya ufisadi wake. JK is a lame duck president, anamaliza kipindi cha mwisho. Hastahili kumhofia Magufuli, lakini bado anamgwaya.

2. Kikwete alitofautiana hadharani na Magufuli kuhusu bomoa bomoa. Wakati Magufuli anataka sheria iwe msumeno, JK anataka ulegelege uendelee.

3. JK hawezi kufanya maamuzi magumu. Hajui tatito la serikali yake liko wapi. Angekuwa kocha wa timu ya mpira, Kikwete unaweza kumfananisha sawasawa na Arsene Wenger ambaye anaona nyumba yake inawaka moto lakini anashindwa kufanya maamuzi magumu ya haraka.

2. P

PROSEKYUTA Member

#2
Aug 25, 2011
Joined: Aug 23, 2011
Messages: 33
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Magufuli ni jembe kweli, kuliko huyo Lowassa mwenye tuhuma lukuki za ufisadi. Ila Kikwete hawezi kamwe kumteua kuwa Waziri Mkuu. Ataweka mtu zezeta tu kama mtoto wa mkulima Pinda

3. Bishop Hiluka

Bishop Hiluka Verified User

#3
Aug 25, 2011
Joined: Aug 12, 2011
Messages: 4,100
Likes Received: 1,424
Trophy Points: 280
Nchi ingenyooka kama angekuwa na Raisi Mkapa na si Rais Kikwete...

4. M

Mojo Senior Member

#4
Aug 25, 2011
Joined: Apr 27, 2011
Messages: 153
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Hapo umenena, Rais legelege hawezi kuteuwa Waziri Mkuu mchapa kazi. Hata ikatokea kwa bahati mbaya kuwa Waziri Mkuu akawa ni mtu mchapa kazi, hawezi kufanya kazi chini ya Rais legelege kama Kikwete. Atakuwa frustrated tu

5. U

ULEVI NOMA Member

#5
Aug 25, 2011
Joined: Jul 31, 2011
Messages: 15
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Samuel Sitta na Harisson Mwakyembe nao wanafaa sana kuwa PM, Pinda ni hovyo kashindwa kazi. Ila tatizo linabaki palepale, Kikwete hawezi kuwa na Waziri Mkuu jembe kwani yeye mwenyewe ni kilaza.

6. S

Simbamwene JF-Expert Member

#6
Aug 25, 2011
Joined: Jun 22, 2008
Messages: 287
Likes Received: 4
Trophy Points: 35
Magufuli aliuza nyumba za serikali O'bay sasa mnataka aueze na Ikulu?

7. Nduka Original

Nduka Original JF-Expert Member

#7
Aug 25, 2011
Joined: Aug 3, 2011
Messages: 753
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Yani wewe ni kipofu kabisa, hivi huyu magufuli si ndo kauza nyumba zetu kwa bei poa au hukumbuki?

8. B

BMT JF-Expert Member

#8
Aug 25, 2011
Joined: Jul 18, 2011
Messages: 570
Likes Received: 94
Trophy Points: 45

inaonekana we n mgeni hee,hakuuza yye hata jk aliridhia,i mean ilkuwa kaul ya pamoja ya serkal ya awam ya tatu chini ya rais mstaafu ben mkapa(rais wa ukwel kwa watanzania mackini)maguful anafaa kuwa PM kwa sasa ,nch iko hovyo kaka,haya we wamtaka nani awe pm?

9. MVUMBUZI

MVUMBUZI JF-Expert Member

#9
Aug 25, 2011
Joined: Jan 8, 2011
Messages: 4,970
Likes Received: 666
Trophy Points: 280
Hawa ndio wametuharibia kabisa dira ya kupambana na ufisadi kwa kujidai wapambanaji kumbe lengo lao lilikuwa kufisha mapambano ya ufisadi na baada ya kufanikiwa wakatunukiwa uwaziri

10. F

FUSO JF-Expert Member

#10
Aug 25, 2011
Joined: Nov 19, 2010
Messages: 11,858
Likes Received: 2,336
Trophy Points: 280
Magufuli hawezi kufanya kazi na JK. ni vitu viwili tofauti kabisa.

11. Nduka Original

Nduka Original JF-Expert Member

#11
Aug 25, 2011
Joined: Aug 3, 2011
Messages: 753
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
edward ngoyai lowasa - mzee wa richmond

12. B

BMT JF-Expert Member

#12
Aug 25, 2011
Joined: Jul 18, 2011
Messages: 570
Likes Received: 94
Trophy Points: 45

namkubali sana lowasa,jk alfanya kosa kubwa kuridhia kujiuzuru kwake,na anguko kubwa la jk lilianzia hapo,namkubali sana tena sana ILA NAONA WAMEMCHAFUA SANA MZEE YULE,NI ZAID YA MAGUFUL KWENYB UWAJIBIKAJI

13. D

DoubleOSeven JF-Expert Member

#13
Aug 25, 2011
Joined: Jul 5, 2008
Messages: 661
Likes Received: 11
Trophy Points: 0
.... very discouraging indeed.
Ndugu, enzi zetu tulithamini sana DHANA YA UONGOZI BORA kwenye usimamizi wa SIASA SAFI kwa WATU wapenda maendeleo. Haya ya personalities za kina Pombe, EL et al ni bure tu bila SERA nzuri. CCM ya leo haina any of that.
Ungetukumbusha kuhusu Katiba mpya kwanza, then useme that all of us (WATU) tutimize wajibu wetu kwa Tanzania in deeds.
Majina mnayotaja sio mwarobaini. As long as adui namba nne, CCM, is in power mvinyo utakuwa ule ule katika chupa na label tofauti.

14. U

Ulimakafu JF-Expert Member

#14
Aug 25, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 18,005
Likes Received: 737
Trophy Points: 280
Si ki hivyo nae ni sehemu ya matatizo ya Tz.

15. ntagunga

ntagunga JF-Expert Member

#15
Aug 25, 2011
Joined: Aug 13, 2011
Messages: 507
Likes Received: 68
Trophy Points: 45
Wtz, tunasahau sana na ni kawaid yetu kulalama. Wadau kumbukeni wakati pinda anaapishwa watu kibao walipongeza na kumpa 5 j.k kuwa kaleta mtu mwadilifu, asiye na tuhuma. Inanishangaza leo wengi wanamponda huyu aliyejitambulisha kuwa mtoto wa mkulima. Kwa ulughai huo, alikubalika sasa anaonekana mwiba. Ni kwamba hata pm awe nani, bado matatizo yatabaki kuwa yaleyale. Iuu

7bu ni kwamba, wote wapo ndani ya mfumo mmoja. Hivyo mfumo ndio unaowatengeneza na kuonekana hawafai. Pendekezo langu ni kwamba, ili tuwe na viongozi imara na shupavu, kwanza mfumo wa utawala uliopo ubadilishwemara moja, then
viongozi wapya waendeshwe na mfumo mpya ambo hautamvumilia mtu mwovu. Kwa sasa hata awe magufuli, bado atamezwa na mfumo na ataonekana kuvunda ndani ya siku chache.

Kama angekuwa kiongozi imara, angejiuzulu wadhifa wake mara baada ya kupingwa stop na wakubwa wake kusimamia sheria halali za nchi. Lkn kwa kuwa na yeye ni sehemu ya mfumo huo, aliendelea kubaki kileleni.

16. l

luckman JF-Expert Member

#16
Aug 25, 2011
Joined: Oct 11, 2010
Messages: 1,202
Likes Received: 174
Trophy Points: 160
nyie wehu kabisa, jambazi linaweza kuendelea kushikilia uwaziri mkuu?????, mwizi ni mwizi tu, magufulI JEMBE!!!!!!!!!!!!!!!

17. Felixonfellix

Felixonfellix JF-Expert Member

#17
Aug 25, 2011
Joined: Feb 16, 2010
Messages: 1,680
Likes Received: 4
Trophy Points: 135
mhhhhhhhhhhhhhhhh
tusubiri tuone

18. Mohammed Shossi

Mohammed Shossi Verified User

#18
Aug 25, 2011
Joined: Jan 17, 2011
Messages: 3,986
Likes Received: 123
Trophy Points: 160
Hivi wale samaki wa magufuli wali cost kiasi gani kuwahifadhi kwenye majokofu ya mmiliki wa vick fish? hivi mhe kwanini hakutumia majokofu ya kwenye meli akaamua kumpatia ulaji mdosi mfanya biashara? kweli ana maamuzi magumu lakini uamuzi wake uliohusu samaki maarufu kama samaki wa magufuli ulinifanya nimfikirie mara mbili ila naamini aliteleza na akipatiwa nafasi hataweza kurudia makosa ya kiufundi kama hayo.

19. Mohammed Shossi

Mohammed Shossi Verified User

#19
Aug 25, 2011
Joined: Jan 17, 2011
Messages: 3,986
Likes Received: 123
Trophy Points: 160
Kuna tetesi kuwa kuna baadhi ya wizara watapewa wapinzani (CDM) na minong'ono inasema ni wizara ya nishati, elimu na pengine uwaziri mkuu patakuwa patamu sana hapo

20. Ibrah

Ibrah JF-Expert Member

#20
Aug 25, 2011
Joined: Mar 22, 2007
Messages: 2,721
Likes Received: 36
Trophy Points: 145

Mudy, Sikutegemea mchango chanya kutoka kwako kwenye hoja hii na bahati nzuri nimethibisha kuwa nilichowaza ni sahihi.

Poor Mnudy!

Loading...