Waziri Mkuu: Jibu sahihi kupunguza changamoto ya ajira ni ujenzi wa viwanda

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,267
2,000
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema mkakati wa Ujenzi wa Viwanda ndio jibu sahihi la kupunguza changamoto ya Ajira Nchini kwa ngazi zote.

Amesema, "Changamoto ya Ajira ipo duniani kote ikiwemo hapa kwetu Tanzania. Kila Serikali inaweka utaratibu mzuri wa kukabiliana nayo"

Ameeleza hayo Bungeni wakati akimjibu Mbunge Nusrat Hanje aliyehoji ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha inawatambua Vijana wanaokwama kupata Ajira kwa kuulizwa kigezo cha Kidato cha Nne.

Mbunge huyo alisema, "Kuna ugumu wa Vijana waliomaliza Darasa la Saba kupata Ajira hususan kwenye Taasisi za Serikali, hata kama wamepata mafunzo katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Ufundi huku kigezo kikiwa ni Cheti cha Kidato cha Nne"

#JamiiForums
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,002
2,000

Waziri Mkuu: Jibu sahihi kupunguza changamoto ya ajira ni ujenzi wa viwanda


Binafsi naona hilo si jibu sahihi ni jibu rahisi​

 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,740
2,000
Ni kweli viwanda vinachukua watu wengi kwa muda mfupi, lakini mpaka viwepo vya kutosha kumaliza tatizo la ajira lililopo itachukua muda mrefu sana.

Nadhani kwanza wangejitahidi kufufua vilivyopo, watafute management nzuri itakayoweza kuvisimamia visife tena, hata ikibidi wataalamu toka nje iwe hivyo.

Hiyo yote ni long term project, short term project wahakikishe wanaiwezesha sekta binafsi, tender nyingi za serikali zitolewe kwa hawa watu kwani wao ndio waajiri wakubwa zaidi ya serikali.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,597
2,000
Hilo lilikuwa jibu enzi za Industrial Revolution..., kipindi hiki cha Automation kiwanda kuwa na wafanyakazi wachache as possible ndio efficiency
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom