Waziri Mkuu ichunguze vizuri Wizara ya Madini, kuna baadhi ya viongozi wa juu wana maslahi katika utendaji wao

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
889
1,000
Mh. Waziri mkuu nimekuandikia huu ujumbe nikiamini wewe au watu wako, au watu wakitengo wataisoma hii na kukufikishia.

Hivi majuzi kunamgodi nimesikia umeibuka maeneo ya mkoa wa SIMIYU kata ya DUTWA kitongoji cha LUBAGA kilicho mpakani mwa wilaya ya Busega na Bariadi.

Baada ya wananchi kuibua machimbo haya ya dhahabu, ziliibuka leseni za watu wakidai niwamiliki halali wa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa mkuu wa mkoa, aliamua kusimamisha leseni hizo, hii nibaada yakutilia shaka uchimbaji huo. Kiujumla wananchi nawadau tulimuunga mkono mkuu wa mkoa kwa sababu zifuatazo.

1. Kumekuwa na janja janja nyingi za watu wenye pesa na viongozi wa wachimbaji wadogo wadogo kujimilikisha maeneo yanayogunduliwa na wananchi, mfano huu mgodi wa lubaga.

Swali la kujiuliza nikwamba , km walikuwa wanamiliki eneo hilo, kwanini hawakulichimba siku zote? Na je, leseni zao walipewa lini? Je, Walifahamika katika ngazi za wilaya, mkoa, kata, tarafa, kijiji na kitongoji kuwa niwamiliki?

Je, walikuwa wamekidhi vigezo vya umiliki wa maeneo hayo kiasi cha kuitwa wamiliki halali wa machimbo hayo nakuanza kutoza mirabaha kwa wachimbaji wale?

TETESI:
Inasadikiwa waziri wa madini mh Dotto Biteko, na KIONGOZI MKUU WA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO kama siyo yeye ni jamaa zake, na baadhi ya tajiri na mtu aliyekaribu na mtoto wa rais aliyemaliza mda wake ambaye ni mkazi wa mkoa huu wa Simiyu, ndio wametengeneza ujanja ujanja huu ambao mkuu wa mkoa aliushtukia nakuamua kusitisha reseni hizo.

Lakini Mh. Waziri Mkuu, kwakuwa waziri wa wizara husika kuwa anawatumia viongozi wa wachimbaji wadogo na watu wenye mitaji mikubwa inasadikiwa yeye alipokuja akawarudisha hao watu wake hizo leseni zilizo simamishwa na Mh Mkuu wa Mkoa.

Maswali niliyoyaweka hapo na mengine ambayo hata wewe utajihoji naamini yatakuongoza wewe mwana JF kulijadiri hili jambo na mh. Waziri mkuu pia anaweza kulichunguza hili jambo km siyo kulifuatiria, au kumchunguza vizuri waziri wa madini na viongozi hao ili kuupata ukweli harisi wa jambo hili, km litakuwa naukweli. ili uwasaidie wananchi wanyonge wanaovumbua madini watambuliwe kama yule mzee wa Tanzanite ambae hakupata kutambuliwa mpaka kipindi hiki cha awamu ya tano kilipoingia madarakani.

Maana siku hizi watu kazi yao nikuwahi kufika eneo na GPS mashine zao na kuwahi kuingiza kwenye systeam ya wizara ambayo mtu mwingine kuingiza taarifa ni mbinde hata kama umefungua porto.

Naomba kuwasilisha tafadhali.

Enzi na Enzi
Dar es salaam.
21 Dec 2020.
 

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
889
1,000
Fatiria leseni zte za uchimbaji na utaftaji nyingi za viongozi wa wachimbaji wadogo wadogo, watu wenye pesa, au jamaa wa makundi haya au viongozi.

Hatukatai km kweli nao wanatafta, lakini siyo walala hoi wakeshe misituni na ndoo zao za maji , hafu wakivumbua wanaishia kubaki na kashimo ambako unaanza kulipa mrabaha wa maroba matatu ya mawe kila maroba kumi.

Mfano hapo lubaga, kunakiongozi wa wachimbaji wadogo wadogo kutoka mkoa wa mara ndio muhusika na ameweka vijana wake kutoka msoma na baadhi ya tajiri wa simiyu mwenye ukaribu na mtoto wa kiongozi mkuu aliyepita.
Huu ni uonevu.
 

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
889
1,000
Kuna chimbo jingine wilaya ya nyang'wale nalo nasikia linataftiwa mtu very soon nalo atapewa mtu wao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom