Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,047
Utangulizi.
Napenda sana kukusalimu kwa heshima kuu na kukupa pole kwa majukumu mazito uliyo nayo ndani ya taifa hili. Napenda kukupongeza kwa kuwa ninaamini wewe ni mmoja wa watu wachache ninaodiriki kusema mnamuelewa sana Mh Raisi. Kwenye hotuba ya Mheshimiwa Raisi katika kumuapisha Naibu Waziri alilalamika sana kuhusu baadhi ya watendaji kutomuelewa juu ya nini hasa anakitaka, lile lilikuwa ni jambo zito sana na napenda kukupongeza kwa kuwa ninajua wewe ni mmoja ya watendaji wanaomuelewa sana Mh. Raisi.
Tatizo na ujenzi/makazi holela.
Napenda nirudi kwenye mada inayohusu dawa ya kumaliza makazi holela hasa kwenye majiji makubwa na mikoa mbalimbali hapa Tanzania ( Dar es Salaam,Iringa,Songwe, Simiyu,Kigoma Mwanza, Morogoro, Singida, Mbeya na Arusha) bila kusahau miji unayokua kama Kahama na mingineyo.
Mh Waziri Mkuu, nadhani unafahamu kuwa kati ya maeneo ambayo kama nchi na taifa tulifeli tangu mwanzo ni kwenye kudhibiti makazi holela. Mfano ni maeneo ya magomeni, tandale, mbagala, gongo la mboto, kimara, temeke, mtoni, tabata na mengineyo mengi.
Lakini vilevile kuna maeneo mapya ambayo kutokana na kuanza kuendelezwa kwa kiwango kikubwa hivi karibuni( Mfano Bunju, Madale, Chanika, Goba, Mbezi Makabe, Kibamba, Kinyerezi, Malamba Mawili n.k) serikali ilitakiwa kuja na mipango madhubuti ili kuhakikisha kuwa ingawa hayajapimwa basi yanajengwa vizuri kama kuhakikisha kuwa at least kwenye kila nyumba ya mtu kunakuwa na barabara inayofika kwake kwa kuwa barabara sio tu zinapendeshesha eneo ila zinaleta mpangilio zaidi na kurahisisha huduma kutolewa kipindi cha majanga kama moto na vilevile kipindi inapotokea mkazi wa eneo husika anaumwa.
Dhumuni la kukuandikia Mh. Waziri Mkuu humu sio kwa sababu simuamini Mh. Lukuvi ila naamini ukilisimamia wewe Mh Lukuvi atalisimamia vizuri na litaleta matokeo chanya. Ninapenda kwa jinsi unavomsaidia raisi wetu mpendwa kwa kuibua changamoto na kuzishughulikia. Nakuomba Mh umsaidie Mh raisi ili aweze kukumbukwa kwenye hili maana makazi holela ni moja ya vitu vinavyoharibu sana picha ya taifa letu.
Nini Kifanyike?
Najua kuna watu wanaweza kusema kuwa dawa la tatizo hili ni makazi kupiwa na kutolewa hati lakini changamoto ninayoiona hapa ni kuwa suala la upimaji limezidi kuwa changamoto kiasi ambacho watu wanazidi kujenga na upimaji umekuwa ukifanyik kwa kiwango cha chini sana. Hivyo Muheshimiwa napendekeza kama serikali mfanye mabadiriko yafuatayo na myatengenezee sera kabisa.
1. Mzipe mamlaka na mzielekeze serikali za mitaa na vijiji kuhusu kupanga maeneo yao( Hasa kwenye maeneo mapya mabayo saivi yameanza kupata uendelezwaji wa kasi sana). Kwenye hili mzielekeze serikali za mitaa na vijiji na watendaji wa kata kuhakikisha kwenye mitaa yao kuna barabara zilizopitishwa zinazohakikisha kila nyumba inapitiwa na barabara yenye uwezo wa kupitisha gari kubwa kama la fire na hata magari wawili kuweza kupishana . Hili likifanyika mtawezesha kupatikana kwa mitaa inayoeleweka na iliyo bora hivo makazi yatawezekana kupangika kiurahisi na hata upimaji utawezekana kiurahisi kama ukija kufanyika badae.
2. Mzielekeze mamlaka na serikali za mitaa na vijiji na watendaji wake kuzisajili barabara zote zilizo kwenye mitaa yao na kuzuia ujenzi wowote kufanyika kuziba barabara izo. Mzipe mamlaka kumvunjia mtu yeyote atakayejenga kwenye baarabara izo zilizosajiliwa
3. Mzipe serikali za mitaa mamalaka ya kusimamisha ujenzi wowote ule unaoonekana unakiuka taratibu za makazi bora kama vile mtu kujenga kwenye mto, njia za maji, kwenye barabara, kuziba njia au kujenga tofauti na mpangilio mzuri uliopo.
Mh waziri Mkuu kama suala la upimaji makazi kabla ya watu kujenga litakuwa gumu napenda kukuhakikishia mkitumia njia hizi hatutakuwa na makazi holela kwa kuwa mkifanya hivi mitaa itapangika vizuri na hata upimaji ukija badae utaweza kurasimisha maeneo ambayo yameshapangika vizuri.
Naomba Kuwasilisha.