Waziri Mkuu hawa Brela wanawaangusha kwenye uwekezaji nchini

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
933
1,000
Wamehama pale jengo la ushirika Lumumba, Wamehamia jengo la Magereza, Sokoine Drive.

Ukifika pale Reception unakutana na vidada viwili, wana kauli mbovu sana,Imewekwa beria wasisogelewe kwa ajili ya Corona. Unapoanza kuelezea shida yako, inabidi upayuke, yeye atakujibu kwa sauti ya chini mno huwezi msikia vizuri, na harudii kukupa ufafanuzi. Usikie usisikie shauri yako anakufokea upishe kwamba ana wateja wengi.

Nimeshuhudia kuna mtu aliaply Usajili online, huyu jamaa amelalamika kwamba issue yake ina zaidi ya Wiki tatu amekuja kuripoti baada ya kutoona Majibu, humohumo ndani amezungushwa siku tatu leo ilikuwa siku ya nne, Uvumilivu ukamshinda akaomba aonane na afisa mwingine badala ya hao waliowekwa reception, amejibiwa Majibu ya jeuri utafikiri wale manesi wa mwananyamala.Amekataliwa haruhusiwi kwenda popote kwa vile kazi yake wanayo wao pale reception, huyu mteja akalalamika kwamba wameshamzugusha sana.

Kuna Dada mmoja mweusi ana kimwili kidogo, huyu Dada hastahili kabisa kuwepo pale ana mdomo mchafu kwa wateja.

Brela ile huduma ambayo huwa mnaitoa kwenye maonyesho ni tofauti kabisa mkifuatwa ofisini kwenu, Mfano ni hao madada hapo reception ambao wanatamani wateja wasifike kabisa kupata huduma hapo.

Mnapoteza pesa za kodi zetu kufanya matangazo kwamba tuepuke kuwatumia madalali wa mtaani ambao hujifanya kwamba wanafanya kazi za kusajili brela, na mnatushawishi tuje ofisini kwenu moja kwa moja. Kwa huduma hizi mbovu hakuna atakayetamani kuja tena ofisini kwenu.

Serikali Inalilia wawekezaji wa nje na ndani nyie mnaikwamisha kwa Huduma zenu mbovu kwenye Usajili wa makampuni. Tafadhali Waziri Mkuu tuma watu wako pale uone kinachofanyika.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,556
2,000
Mambo kama haya Magufuli alijitahidi kuyakomesha lakini wapi, alishindwa ingawa aliyapunguza. Watanzania tabia hii ya huduma mbovu kwa wateja ipo kwenye damu au niseme DNA yetu.

Sasa kaingia Mh.Samia wanamchafua kwa vile siyo mkali wamerudi enzi za JK na kurudi kunyuma zaidi. Mama watumbue waje mtaani waone maisha yalivyo watakuheshimu, wataheshimu kazi zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom